Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya: Wakwepa kodi sasa kunaswa kwa Kamera

KRA Camera Wakwepa kodi sasa kunaswa kwa Kamera

Wed, 22 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka ya Mapato Kenya (KRA) imesema itaanza kutumia kamera zitakazovaliwa na wafanyakazi wake ili kushughulikia wizi wa ushuru na rushwa, mkuu wa KRA amenukuliwa na gazeti la Business Daily la nchini humo.

Kamera hizo zitatumiwa hasa na wafanyikazi wa ndani katika idara ya kodi na wale wa udhibiti wa forodha na mipaka, kwa mujibu wa ripoti hiyo.

Baadhi ya wafanyakazi wa KRA wameshutumiwa kwa kujilimbikizia mali ambazo haziendani na malipo yao.

"Hivi karibuni pia tutahakikisha maafisa wetu wana kamera zilizovaliwa kama hizi unazoziona huko Marekani, ili hatua yoyote watakayochukua irekodiwe na sisi tuione. Ukiizima, pia tutaelewa ni kwa nini unafanya hivyo," Kamishna Mkuu wa KRA Githii Mburu alinukuliwa akisema.

Mwaka jana, mamlaka ya ushuru ilitangaza kuwa inatazama wasifu wa mitandao ya kijamii wa watu waliolengwa ili kulinganisha mtindo wao wa maisha na ulipaji wao wa kodi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live