Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya: Wakazi wa Siaya wanufaika na mradi wa Solar

Umeme Jua Solar.png Kenya: Wakazi wa Siaya wanufaika na mradi wa Solar

Wed, 28 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kisiwa cha Ndeda katika kaunti ya Siaya, Magharibi mwa nchi ya Kenya kimekuwa gizani tangu ukoloni, kutokana na umbali na nchi kavu hali ambayo imekuwa ngumu kufikisha miundombinu ya nishati.

Hata hivyo tangu mradi wa Solar ulipozinduliwa kisiwani humo miaka 6 iliyopita, mabadiliko makubwa yameanza kushuhudiwa.

Safari ya kufika hapa imechukua muda wa saa moja na nusu kutoka pwani ya Uyawi, eneo la Bondo kaunti ya Siaya.

Hapa wakaazi wanaendela na shughuli zao za kusaka riziki, kinyume na ilivyokuwa miaka ya nyuma, sasa hali ya maisha imebadilika kutokana na mradi huu ambao unatumika kusambaza umeme hapa. James Mbago ni mkaazi wa eneo hili.

“Tangu watuletee solar tumekuwa na afueni” alisema James Mbago.

Katika zahanati ya Ndeda nakutana na kina mama ambao wamewaleta watato wao kupata matibabu. Zahanati hii inafanya kazi saa 24 hali ambayo wakaazi wanaona ni fahari.

“Zamani ilibidi usubiri mpaka asubuhi kwa sababu usiku ilikuwa ni vigumu.” Walisema baadhi ya akina mama katika eneo hili.

Kulingana na Daktari Arthur Oda, ambaye alikuja hapa mwaka 2011, kabla ya mradi huu, ameshuhudia mabadiliko makubwa katika hospital hii.

“Kitambo kulikuwepo na shida sana haswa kwa upande wa akina mama waliokuwa wanatafuta huduma za matibabu saa za usiku.” alieleza daktari Arthur Oda. Daktari Oda anawahudumia wagonja usiku na mchana, kwakuwa serikali ya kaunti ime mpa makazi katika eneo hili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live