Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya: Waandamanaji walirushiwa gesi ya kutoa machozi nje ya kituo cha polisi

Kenya: Waandamanaji Walirushiwa Gesi Ya Kutoa Machozi Nje Ya Kituo Cha Polisi Kenya: Waandamanaji walirushiwa gesi ya kutoa machozi nje ya kituo cha polisi

Sun, 9 Jul 2023 Chanzo: Bbc

Polisi nchini Kenya wamefyatua mabomu ya machozi kuwatawanya wanaharakati wa haki za binadamu wanaotaka kuachiliwa kwa makumi ya watu waliokuwa wakizuiliwa wakati wa maandamano ya kuipinga serikali siku ya Ijumaa.

Kanda za video zinaonyesha moshi wa gesi ya kutoa machozi katika kituo kikuu cha polisi cha Nairobi.

Miongoni mwa waandamanaji wa leo ni aliyekuwa Jaji Mkuu Willy Mutunga.

Kiongozi wa upinzani Raila Odinga aliitisha maandamano ya Ijumaa kupinga kupanda kwa ushuru wa mafuta na gharama ya juu ya maisha.

Takriban mtu mmoja anaripotiwa kuuawa wakati polisi walipojibu maandamano katika miji ya Nairobi, Mombasa na Kisumu.

Takriban watu 28 walikamatwa.

Chanzo: Bbc