Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya: Waandamanaji 174 wakamatwa na polisi

Maandamano Kenya Ghsz Kenya: Waandamanaji 174 wakamatwa na polisi

Fri, 9 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Polisi nchini Kenya imewakamata watu 174 nchi nzima wakati wa maandamano ya kupinga serikali yaliyofanyika siku ya Nanenane kulingana na taarifa ya Kaimu Inspekta Jenerali wa Polisi Gilbert Masengeli.

Akihutubia wanahabari katika Jumba la Jogoo jijini Nairobi jioni ya siku ya Alhamisi, Masengeli amebainisha kuwa maandamano hayo yalirekodi idadi ndogo ya waliojitokeza huku kukiwa na visa vidogo vya uporaji na uharibifu wa mali.

"Tofauti na maandamano ya hivi majuzi ambayo yalikumbwa na uharibifu wa mali, uporaji, majeraha na kupoteza maisha, leo hii nchi imesalia kuwa ya amani na ya hali ya kawaida, isipokuwa Nairobi ambapo afisa mmoja alijeruhiwa”, alisema Kaimu wa Polisi IG.

Bosi huyo wa polisi ameendelea kubainisha kuwa waandaaji wa maandamano ya Nane Nane walishindwa kuvijulisha vyombo vya usalama kuhusu hatua walizopanga kama ilivyoainishwa katika sheria.

Hata hivyo, amebainisha kuwa maafisa wa polisi walikuwa na jukumu hilo na walitumwa ipasavyo ili kuhakikisha hakuna machafuko yanayoshuhudiwa kama vile upelelezi ulivyoonesha.

"Licha ya kushindwa kwa waandaaji wa maandamano ya leo kuwajulisha Polisi kuhusu nia yao ya kufanya maandamano, tulihakikisha kwamba wana usalama wa kutosha na kuwatahadharisha wananchi kuepuka maeneo yenye msongamano ambayo yanaweza kugeuka kuwa na ghasia”, alionya Masengeli.

Siku ya Jumatano, Masengeli alionya kwamba maandamano ya Alhamisi yanaweza kupenyezewa wahuni, na kutishia usalama wa nchi.

"Maandamano ya awali yaliyofanyika mwezi Juni yalikuwa ya amani lakini maandamano yaliyofuata yalibadilika na kuwa ghasia, huku waporaji wakiharibu na kuiba mali," alisema.

Mbali na kuwataka wananchi kuwa waangalifu wakati wa maandamano hayo, Masengeli vilevile alionya waandamanaji dhidi ya kuvamia ardhi iliyolindwa kama ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) na Ikulu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live