Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya: Takwimu matukio ya Uingereza kwa jamii ya Wamasai..

Fidia Kenyaaaaaaaaaaaa Kenya: Takwimu matukio ya Uingereza kwa jamii ya Wamasai

Mon, 30 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakenya wametoa wito wa kutendewa haki kutokana na uhalifu uliofanywa na wanajeshi wa Uingereza nchini humo miaka kadhaa iliyopita.

Wito huo umetolewa kabda la safari ya Mfalme Charles nchini Kenya, Jumanne ya kesho.

Ziara ya Mfalme wa Uingereza nchini Kenya nawakumbusha Wakenya mambo machungu zaidi ya historia ya ukoloni wa Wazungu nchini kenya na barani Afrika kwa ujumla.

Mwezi Agosti mwaka huu, Bunge la Kenya lilianzisha uchunguzi kuhusu ripoti za ukiukaji wa haki za binadamu na ukiukwaji wa maadili unaofanywa na kitengo cha mafunzo cha jeshi la Uingereza ambacho kwa miongo kadhaa kimeweka kambi nchini Kenya.

Kila mwaka karibu wanajeshi 10,000 Uingereza hupata mafunzo katika kambi maalumu iliyo katika kaunti ya Laikipia.

Wakenya wameibua wasiwasi kuhusu jinai za majeshi ya Uingereza dhidi ya wakazi wa eneo hilo na pia uharibifu mkubwa wa mazingira ikiwa ni pamoja na uteketezaji misitu ya jadi.

Mwishoni mwa 2021, polisi wa Kenya walisema wanafungua tena kesi ya mwanamke wa eneo hilo, Agnes Wanjiru, ambaye ilisemwa kuwa aliuawa na mwanajeshi wa Uingereza mwaka wa 2012.

maiti ya Wanjiru aliyekuwa na umri wa miaka 21, mama wa binti wa miaka miwili, iligunduliwa kwenye tanki la majitaka huko Nanyuki.

Kisa cha kusikitisha cha Agnes Wanjiru kilitonesha kidonda cha machungu yaliyosababishwa na utawala wa kikoloni wa Uingereza nchi Kenya.

Mnamo Oktoba 2021, gazeti la Uingereza la The Sunday Times liliripoti kwamba mwanajeshi mmoja wan chi hiyo alikiri kwa wenzake kumuua Wanjiru, na kuwaonyesha mwili wake.

Ripoti hiyo ilisema kuwa Habari ya mauaji hayo iliripotiwa kwa wakuu wa jeshi, lakini hakuna hatua zaidi iliyochukuliwa.

Mwaka wa 2003, shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International liliripoti kuwa limesajili madai 650 ya ubakaji dhidi ya wanajeshi wa Uingereza waliokuwa katikati mwa Kenya kati ya 1965 na 2001, na "miongo kadhaa ya kukwepa adhabu" serikali ya London.

Wabunge wa Kenya mwezi Aprili waliidhinisha mkataba mpya wa ushirikiano wa miaka mitano wa ulinzi na Uingereza na pia walipendekeza kuruhusu wanajeshi wowote wa Uingereza walioshtakiwa kwa mauaji kuhukumiwa nchini humo.

Mwenyekiti Kamati ya Bunge ya Ulinzi, Ujasusi na Mahusiano ya Kigeni ya Bunge la Kenya, Nelson Koech, alisema katika taarifa mapema mwaka huu kwamba uchunguzi huo "utatoa fursa kwa Wakenya waliotatizika kupata haki, na kwamba hii itakuwa nguzo muhimu kwa azimio la kamati hiyo kuhakikisha wanajeshi wa Uingereza ambao wanakiuka sheria katika ardhi ya Kenya wanafikishwa kizimbani."

Katika safari yake ya siku nne nchini Kenya, Mfalme Charles wa Uingereza anatazamiwa kuzuru Nairobi na Mombasa; sio Nanyuki ambapo wanajeshi wa Uingereza wameweka kambi.

Mnamo Oktoba 20, wawananchi walifanya maandamano katika mji huo wakidai fidia kutokana na uhalifu uliofanywa na jeshi la Uingereza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live