Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya: Shughuli za kiuchumi zimeongezeka katika kisiwa cha Ndeda

Umeme Jua Solar.png Kenya: Shughuli za kiuchumi zimeongezeka katika kisiwa cha Ndeda

Wed, 28 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shughuli za kiuchumi zimeongezeka katika kisiwa cha Ndeda kwenye Ziwa Victoria, katika kaunti ya Siaya, Magharibi mwa nchi ya Kenya tangu kiwekewe huduma za sola.

Nyumba za waakazi katika kisiwa hiki zimepangwa sawia na mitaa ya mabanda kwani zimejengwa na mabati, Kila sehemu utakutana na wafanyibishara wa rejareja au wachuuzi.

Aidha Biashara zinazotumia nguvu za umeme hazikosi, Nicholas Omondi pamoja na Sammuel Otieno wanafanya biashara ya kinyozi na tangu waanzishe biashara hii, hawajajutia.

“Tumefaidika sana maana zamani tulikuwa tunatumia sola zetu kisha usiku hakuna kazi maana hakuna jua ila sasa tunafanya kazi hadi muda wa usiku tangu sola hizo zije.” Walisema wafanyibiashara hawa.

Moja ya biashara kubwa zaidi katika kisiwa hiki, ni uvuaji wa samaki, japo kwa sasa kina ushindani mkubwa, Osman Hassan ambaye usafirisha samaki nje ya kaunti hii anasimulia jinsi ambavyo anahifadhi samaki wake.

“Kwa sasa tunahifadhi samaki wetu kwenye jokovu kwa siku kadhaa kabla kusafirisha na hawaharibiki.” alieleza Osman Hassan.

Na kwa kuwa hakuna kizuri kisicho na dosari, kuna baadhi ya wakaazi bado wanaomba msaada licha ya juhudi za wafadhali wa mradi huu kuwawezesha kuwa na huduma za sola kwa gharama ya chini. Elly Ouma ni mwenyekiti wa Bodi ya wavuvi katika eneo hilo.

Kila mara boti inapotia nanga hapa, bila shaka ni mwanzo wa pilka pilka za kupakua bidhaa za biasha ili kuimarasha uchumi wa kisiwa cha ndeda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live