Waziri wa mambo ya ndani nchini Kenya Kithure Kindiki amekanusha madai kwamba maafisa wa polisi walitumwa kumkamata waziri wa zamani wa mambo ya ndani Fred Matiang'i nyumbani kwake usiku wa Jumatano.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari Bw. Kindiki alisema madai hayo ni ya uwongo.
"Tumepokea ripoti za vyombo vya habari kuhusu madai ya uvamizi wa makazi ya waziri waziri wa zamani wa mambo ya ndani Dr. Fred Matiang’i’ na watu wasiyojulikana jana usiku'.
“Mawakili wa Dkt. Matiangi na baadhi ya wanasiasa waliozungumza kutoka eneo la tukio walidai kuwa watu hao walikuwa maafisa wa polisi waliotumwa kumkamata aliyekuwa Katibu wa Baraza la Mawaziri.
"Madai haya ni ya uongo mtupu. Hakuna afisa wa polisi au ajenti yeyote wa usalama kutoka taasisi au idara yoyote ya Serikali aliyetumwa nyumbani kwa Dk. Matiang'i kumkamata, kumnyanyasa au kuingilia haki zake za Kikatiba kwa namna yoyote ile," Kindiki alisema.