Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya: Serikali yaelekeza ukaguzi wa mabwawa yote

Kenya:Serikali Yaelekeza Ukaguzi Wa Mabwawa Yote Kenya: Serikali yaelekeza ukaguzi wa mabwawa yote

Mon, 29 Apr 2024 Chanzo: Bbc

Serikali nchini Kenya imeagiza Kamati za Usalama na Ujasusi za Kaunti kote nchini humo kukagua mabwawa yote ya umma na ya kibinafsi kufikia keshoJumanne.

Waziri wa Usalama wa Ndani Kithure Kindiki mnamo Jumatatu aliagiza kamati hizo kupendekeza baadaye kutolewa kwa amri za kuhamisha watu kwa lazimakatika makazi yanayochukuliwa kuwa katika hatari hadi maeneo salama.

Haya ni kufuatia kisa cha Jumatatu asubuhi ambapo bwawa lilipasua kingo zake huko Mai Mahiu, Kaunti ya Nakuru, na kuzisombanyumba na magari, na kuwaua zaidi ya watu 42.

Mafuriko hayo yalitoka kwenye mto ulio karibu ambao ulivunja kingo zake baada ya mvua kunyesha, kulingana na Shirika la Msalaba Mwekundu.

Waziri wa Mambo ya Ndani aliagiza kaunti kupeleka vikosi vya kutekeleza sheria katika maeneo ya barabarani ambayo hukabiliwa na mafuriko na na katika sehemu zadaraja ili kuzuia madereva au watembea kwa miguu kuhatarisha maisha yao kwa kuvuka.

Chanzo: Bbc