Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya: Rais Ruto kuzuru nchi ya Japan

Ruto Japan Japna.png Kenya: Rais Ruto kuzuru nchi ya Japan

Mon, 5 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Kenya William Ruto, hapo kesho Jumanne anatarajiwa kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili nchini Japan.

Ziara hii imekuja baada ya waziri mkuu wa Japan Fumio Kishida kuzuru Nairobi mwaka uliopita wakati akiwa katika ziara ya siku nne barani Afrika ambapo alitembelea nchi za Misri, Kenya, Ghana na Msumbiji.

Ziara hiyo ya kidiplomasia inatarajiwa kuimarisha ushirikiano kati mataifa hayo mawili, Nairobi ikitarajiwa pia kuboresha uchumi wake kupitia uhusiano baina yake na Tokyo.

Safari ya mkuu wa nchi imethibitishwa na mkuu wa mawaziri katika taifa hilo la Afrika Mashariki Musalia Mudavadi ambaye pia ni waziri wa mambo ya kigeni wa Kenya.

Kwa mujibu wa waziri Mudavadi, viongozi hao wawili wanatarajiwa pia kujadiliana kuhusu masuala ya umuhimu kwa nchi zao ikiwemo ushirikiano wa kiuchumi, elimu, ufadhili wa masomo, miundombinu pamoja na usalama wa kikanda haswa katika mataifa ya Afrika Mashariki.

Aidha Mudavadi ameleza kuwa nchi ya Japan imefadhili baadhi ya miradi mikubwa nchini kenya haswa katika sekta ya afya, ukulima na elimu.

Licha ya kukoselewa kwa kufanya safari nyingi za kigeni, Musalia Mudavadi amemtetea rais Ruto, akieleza kwamba ziara hizo katika nchi za kigeni zilikuwa zinaleta manufa kwa raia wa Kenya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live