Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya: Mshukiwa wa mauaji ya wanawake 42 atoroka gerezani

Kifo Kifo Mauiaji.png Kenya: Mshukiwa wa mauaji ya wanawake 42 jijini Nairobi atoroka gerezani

Tue, 20 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Raia wa Kenya aliyekiri kuhusika na mauaji ya wanawake 42 ambao baadhi yao miili yao ilipatikana imetupwa katika eneo la kutupa taka jijini Nairobi, ametoroka gerezani.

Ameripotiwa kutoroka gerezani pamoja na wafungwa wengine kwa mujibu wa taarifa ya polisi.

Collins Jumaisi, 33, alikamatwa na polisi mwezi uliopita baada ya miili ya wanawake waliokatakatwa vipande kupatikana ikiwa imetupwa kwenye eneo la taka katika mtaa wa Embakasi, nje kidogo na jiji la Nairobi.

Kwa mujibu wa msemaji wa polisi nchini Kenya, wafungwa 13 walitoroka gerezani usiku wa kuamkia Jumanne ya wiki hii, akiwemo mshukiwa mkuu wa mauaji ya wanawake hao.

Miongoni mwa wafungwa waliotoroka gerezani ni pamoja na raia 13 wa Eriteria kulingana na taarifa ya msemaji wa polisi.

Jumaisi alikuwa aliwasilishwa mahakamani Ijumaa ya wiki iliopita ambapo hakimu aliagiza azuiliwe kwa muda wa miezi 30 zaidi kutoa nafasi ya uchunguzi kukamilika.

Miili 10 ya wanawake waliokuwa wamekatwa katwa ilipatikana ikiwa imefungwa kwenye mifuko ya plastiki na kutupwa kwenye eneo la taka katika mtaa wa Mkuru kulingana na ripoti ya shirika la kutetea haki za binadamu mwezi uliopita.

Jumaisi alikamatwa tarehe 15 ya mwezi Julai karibu na eneo la burudani ambapo alikuwa akifuatilia michezo ya Euro 2024.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live