Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya: Mkuu wa majeshi ya ulinzi Jenerali Francis Ogola alikuwa nani?

Kenya Mkuu Majeshoi Nani.png Kenya: Mkuu wa majeshi ya ulinzi Jenerali Francis Ogola alikuwa nani?

Fri, 19 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kupitia mtandao wake wa kijamii wa X, ametuma salamu za pole kwa Wakenya kufuatia kifo cha Mkuu huyo wa Majeshi ya Kenya, salamu ambazo pia zimetumwa na Mkuu wa Tume ya Umoja wa Afrika Mousa Faki, Jumuiya ya IGAD na ubalozi wa Marekani na Uingereza nchini Kenya.

Jenerali Ogola aliteuliwa na rais William Ruto kwenye nafasi hiyo mwezi Aprili mwaka uliopita, akitokea kwenye jeshi la angaa.

Hadi kifo chake, alikuwa na umri wa miaka 61, ambapo alikuwa anaelekea kutimiza mwaka mmoja kwenye nafasi hiyo na kustaafu mwaka ujao kwa mujibu wa utaratibu wa kijeshi.

Mzaliwa wa Kaunti ya Siaya, Magharibi mwa Kenya, Jenerali Ogola alijiunga na Jeshi la Kenya tarehe 24 mwezi Aprili mwaka 1984.

Kabla ya kuwa Mkuu wa Majeshi ya ulinzi, Jenerali Ogola ambaye alisomea Sayansi ya Kijeshi kutoka chuo École Militaire de Paris nchini Ufaransa, na vyuo vingine nchini Kenya, aliwahi pia kuhudumu kama rubani na mkufunzi wa ndege za kijeshi.

Cheo cha Mkuu wa Majeshi ya ulinzi ya Kenya maarufu kama CDF ndicho cha juu katika ngazi ya kijeshi nchini humo na kushikiliwa na Jenerali anayeteuliwa na rais aliye madarakani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live