Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya: Mjadala waibuka kuhusu hatma ya hukumu ya kifo

Hukumu Pc Data Kenya: Mjadala waibuka kuhusu hatma ya hukumu ya kifo

Thu, 21 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nchini Kenya, mjadala umeibuka kuhusu hatma ya hukumu ya kifo inayoendelea kutolewa na mahakama licha ya kuwa taifa hilo halijanyonga mfungwa yeyote tangu mwaka 1987.

Wiki iliyopita mahakama kuu ilimuhukumu kuonyongwa hadi kufa Joseph Jowie Irungu kwa mauaji ya mfanyibiashara Monica Kimani.

Lakini kwa nini adhabu hii inaendelea kutolewa licha ya kutotiwa saini na Rais kutekelezwa? Mwandishi wetu Douglas Omariba anaeleza zaidi.

Jaji wa mahakama ya rufaa Luka Kimaru anasema hukumu hiyo iko kwenye katiba na ni jukumu la Rais kutia saini wanyongwe.

“Mahakama ikishahukumu mtu kifo, Rais anafaa kutia sahihi karatasi ya kusema anyongwe. Rais Moi hakufanya hivyo sawa na Rais Kibaki na Uhuru.” alisema Jaji wa mahakama ya rufaa Luka Kimaru.

Ni uamuzi ambao hata hivyo haukupokelewa vizuri na Elijah Kandie kutoka tume ya kitaifa ya haki za kibinadamu nchini Kenya.

“Kulingana na mtazamo wetu, adhabu ya kifo ni ukiukaji wa mwisho wa haki za kibinadamu.” alieleza Elijah Kandie.

Mchanganuzi wa masuala ya usalama George Musamali anasema adhabu ya kifo haijakuwa suluhu kwa uhalifu.

“Licha ya kuwa adhabu ya kifo ipo, makossa ya jinai yanaendelea kutekelezwa na kufika mahakamani adhabu ya kifo inatolewa.” alieleza Mchanganuzi wa masuala ya usalama George Musamali. Aidha, wananchi nchini humo wana maoni tofauti.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live