Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya: Miili ya watu waliofariki Shakahola kutolewa kwa familia

Kenya: Miili Ya Watu Waliofariki Shakahola Kutolewa Kwa Familia Kenya: Miili ya watu waliofariki Shakahola kutolewa kwa familia

Tue, 26 Mar 2024 Chanzo: Bbc

Familia za waathiriwa wa mauaji ya Shakahola yaliyotokana na dhehebu la funga hadi ufe zimekusanyika katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Malindi pwani ya Kenya kuchukua miili ya jamaa zao.

Miili 34 pekee ndiyo iliyolinganishwa na familia.

Mabaki hayo ni ya kwanza kukabidhiwa kwa familia zao baada ya takriban mwaka mmoja wa shughuli kibwa ya kuwatambua kwa kutumia DNA.

Mamia ya miili, ikiwa ni pamoja na ya watoto, ilifukuliwa kutoka kwenye makaburi ya halaiki ya kina kirefu yaliyogunduliwa mwezi Aprili mwaka jana katika msitu wa Shakahola.

Chanzo: Bbc