Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya: Miaka 10 baada ya shambulio la kigaidi Westgate

Wastage Mall Shabaab.png Kenya: Miaka 10 baada ya shambulio la kigaidi Westgate

Thu, 21 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Leo ni miaka 10 tangu wapiganaji wa Al Shabab kuvamia jengo la kibiashara katika eneo la Westlands jijini Nairobu na kuwaua watu 67. Mashambulio hayo ya kigaidi bado ni tishio nchini Kenya.

Shambulio hilo lilitokea jumamosi saa sita, na kudumu kwa siku nne, watu 67 wakiwauwa na wengine 200 wakijeruhiwa.

Watu wenye silaha, walivamia jengo hilo la Westgate lilokuwa na orofa nne, wakipiga risasi mfululizo na kurusha magureneti.

Kulikuwa na mashindano ya mapishi ya watoto kwenye orofa ya juu, hivyo watoto wengi walipoteza maisha.

Baada ya shambulio hilo, Kenya imeshuhudia mashambulio mengine likiwemo shambulio kwenye chuo kikuu cha Garissa ambapo wanafunzi zaidi ya mia waliwauwa,shambulio la hotel ya Dusit mwaka 2019 watu 21 wakiwauwa.

Maeneo ya kaskazini mashariki na Pwani ya Kenya, haswa Lamu bado yameendelea kulengwa na Al Shabab hadi sasa, hatua ambayo imemlazimu waziri wa usalama wa ndani Kithuri Kindiki kutangaza kuwatuma vikosi maalum maeneo hayo.

‘‘Tutaweka vikosi maalum kutoka kwa maofisa wetu spesheli ambao wamepokea mafunzo maalum ya kupambana na magaidi sugu.’’ alisema waziri Kindiki.

Kenya iliamua kuwatuma wanajeshi Wake nchini Somalia mwaka 2011, uamuzi ambao umeifanya kuwa shabaha ya Al Shabab.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live