Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya: Mchungaji Mackenzie amefunguliwa mashtaka ya mauaji

Pia Wewe Utakufa Siku Moja Mackenzie Amwambia Hakimu Kenya: Mchungaji Paul Mackenzie amefunguliwa mashtaka ya mauaji

Wed, 24 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Paul Mackenzie Mchungaji mwenye utata anayedaiwa kuwashawishi wafuasi wake zaidi ya 200 kufunga hadi kufa ili kwenda mbinguni mwaka uliopita, Pwani ya Kenya amefunguliwa mashtaka ya mauaji yeye pamoja na washukiwa wengine zaidi ya 90.

Mackenzie na washukiwa wenzake, akiwemo mke wake, wamekanusha mashataka yote 238 yakiwemo ya mauaji yanayowakabili mbele ya Mahakama ya mji wa Malindi.

Hatua hii inakuja baada ya viongozi wa mashtaka wiki iliyopita kumfungulia Mackenzie mashtaka mengine ya ugaidi, kwa kuwashawishi wafuasi wake kufunga chakula hadi kufa ili wamwone Yesu.

Mchungaji huyo na wafuasi wake, walikamatwa mwezi Aprili mwaka uliopita, baada ya miili ya watu kupatikana katika msitu wa Shakahola, wakiwemo watoto na wanawake.

Wakati kesi dhidi yake ikianza, Mahakama imeelezwa kuwa watu 238 walipoteza maisha kati ya Januari 2021 hadi Septemba 2023 baada ya kupewa mafunzo ya kupotosha na mchungaji huyo. Mahakama imetaka Mackenzie kupimwa akili, wakati huu kesi ikianza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live