Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya: Mahakama yasitisha utekelezaji wa mpango mpya wa bima ya afya

Kenya:Mahakama Yasitisha Utekelezaji Wa Mpango Mpya Wa Bima Ya Afya Kenya:Mahakama yasitisha utekelezaji wa mpango mpya wa bima ya afya

Tue, 28 Nov 2023 Chanzo: Bbc

Mahakama moja nchini Kenya imesitisha utekelezaji wa Sheria ya Bima ya Afya ya Jamii ya mwaka 2023 hadi Februari 7, 2024.

Jaji Chacha Mwita alitoa agizo hilo katika kesi iliyowasilishwa na mwanaharakati Joseph Aura na Muungano wa Madaktari wa Kenya (KMPDU) na Chama cha Madaktari cha Kenya (KMA) walioorodheshwa kama wahusika.

"...agizo linatolewa kuwazuia(Rais William Ruto, Mawaziri katika Wizara ya Afya , Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mamlaka ya ukusanyaji Mapato, Bunge la Kitaifa na Seneti), maajenti wao na au mtu yeyote juu ya maagizo yao ya kutekeleza Sheria ya Bima ya Afya ya Jamii, 2023; Sheria ya Afya ya Msingi, 2023 na Sheria ya Afya ya Kidijitali, 2023 hadi Februari 7, 2024," aliagiza Mwita.

Zaidi ya hayo, mahakama iliwapa walalamishi siku saba kuwasilisha majibu yao.

Wiki iliyopita, matabibu walikosoa Sheria ya Afya ya Kijamii wakisema ni ukiukaji wa Makubaliano ya Pamoja ya mwaka 2017 (CBA) kuhusu utoaji wa bima ya kina ya matibabu na mwajiri.

Katibu Mkuu wa Muungano wa Madaktari Wafamasia na Madaktari wa Meno nchini Kenya Davji Bhimji alidokeza kuwa Sheria hiyo ilikuwa ya kibaguzi kwa Watumishi wa Umma na Wakenya kwa ujumla.

Chanzo: Bbc