Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya: Mafuriko yaongeza hatari ya ugonjwa wa kipindupindu

Kenya: Mafuriko Yaongeza Hatari Ya Ugonjwa Wa Kipindupindu Kenya: Mafuriko yaongeza hatari ya ugonjwa wa kipindupindu

Wed, 8 May 2024 Chanzo: Bbc

Maambukizi 44 vya kipindupindu vimeripotiwa katika kaunti ya Tana River nchini Kenya, huku mafuriko yakiongeza hatari ya kuenea kwa magonjwa yanayotokana na maji.

Taarifa ya Shirika la Afya Duniani (WHO) ambayo inataja idadi hiyo, inasema maafisa wa Kenya wanaoshirikiana na WHO na mashirika mengine wamekuwa wakifuatilia hali ya afya na mwitikio kote nchini humo kutokana na mafuriko.

Mafuriko hayo yameathiri zaidi ya watu robo milioni huku vifo 238 vimeripotiwa kote nchini. Tana River ni mojawapo ya kaunti zilizoathiriwa zaidi na mafuriko.

Siku ya Jumanne, Katibu Mkuu wa Afya wa Kenya Mary Muthoni alisema kuna hatari kubwa ya magonjwa yanayosambazwa na maji kuwa janga ikiwa hayatashughulikiwa kwa wakati.

Bi Muthoni alizungumza huku yeye na maafisa wengine wa afya wakisambaza bidhaa za kusafisha maji katika mji mkuu, Nairobi.

Pia alielezea hatari ya magonjwa kutokana na uchafuzi wa chakula na vyanzo vya chakula visivyo salama ambavyo vinazidishwa na mafuriko.

WHO inasema itaendelea kuunga mkono hatua za dharura za serikali na "kuwa macho kwa milipuko ya magonjwa ambayo inaweza kuenea kwa urahisi ikiwa haitadhibitiwa haraka".

Chanzo: Bbc