Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya: Mafuriko yanaendelea kuripotiwa katika baadhi ya maeneo

Mks Mafuriko Kenya: Mafuriko yanaendelea kuripotiwa katika baadhi ya maeneo

Mon, 20 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Milii ya maofisa wawili wa halmashauri ya ukusanyaji ushuru nchini Kenya, ambao walikuwa wamesombwa na mafuriko wakati wakiwa safarini pwani ya Kenya Ijuma iliyopita, imepatikana hapo jana Jumapili.

Haya yanajiri wakati huu mamlaka ikithibitisha kuwa watu 10 wamefariki kutokana mafuriko yanayoendelea pwani ya taifa hilo la Afrika Mashariki, mafuriko ambayo yamesababishwa na mvua kubwa inayoendelea kunyesha.

Kwa mujibu wa kamishena wa polisi katika eneo la pwani ya Kenya, Rhoda Onyancha zaidi ya familia elfu 20 zimepoteza makazi yao katika kaunti za Mombasa, Kilifi, Kwale na Tana River kutokana na mafuriko.

Watu kadhaa wamethibitishwa kufariki katika maeneo tofauti ya nchi, wakati maelfu ya wengine wakiripotiwa kupoteza makazi yao tangu kuaanza kwa mvua kubwa mwanzoni mwa mwezi Novemba.

Mvua kubwa pia imeripotiwa kusababisha mafuriko ambayo yamewaua watu kadhaa katika nchi jirani za Somalia na Ethiopia.

Takwimu za shirika la msalaba mwekundi nchini humo zinaonyesha kuwa zaidi ya watu eflu 58 wameathiriwa na mafuriko hayo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live