Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya Kwanza yataja wawakilishi wake katika mazungumzo na Azimio

Kenya Kwanza Yataja Wawakilishi Wake Katika Mazungumzo Na Azimio Kenya Kwanza yataja wawakilishi wake katika mazungumzo na Azimio

Tue, 11 Apr 2023 Chanzo: Radio Jambo

Muungano wa Kenya Kwanza umewataja viongozi watakaowakilisha serikali katika mazungumzo na upinzani.

Seneta wa Kakamega, Boni Khalwale ndiye atakayewaongoza viongozi hao katika mazungumzo hayo.

Timu hiyo ya wajumbe saba inajumuisha wabunge wanne wa Bunge la Kitaifa na Maseneta watatu.

Hii hapa orodha kamili:

1. Boni Khalwale -Seneta wa Kakamega

2. George Murugara - Mp Tharaka

3. Esther Okenyuri - Seneta Mteule

4. Mwangi Mutuse -Mbunge Kibwezi Magharibi

5. Lydia Haika -Mwakilishi wa Wanawake Taita Taveta

6. Hillary Sigei-Seneta Bomet

7. Adan Keynan - Mbunge Eldas

Timu hiyo itashiriki mazungumzo ya vyama viwili pamoja timu ya wanachama saba ambao walitangazwa na kiongozi wa muungano wa Azimio la Umoja- One Kenya Raila Odinga wiki jana.

Saba hao ni pamoja na Seneta wa Nairobi na ambaye ni katibu mkuu wa ODM Edwin Sifuna, Seneta wa Narok Ledama Ole Kina na Seneta wa Kitui Enoch Wambua. Wabunge wengine ni Otiende Amollo (Rarieda), David P'Kosing (Pokot Kusini), Millie Odhiambo (Suba Kaskazini) na Amina Mnyanzi (Malindi).

Timu hiyo ilichaguliwa wakati wa mkutano wa kikundi cha wabunge wa Azimio la Umoja katika Kaunti ya Machakos.

Hii ilikuwa baada ya Raila kukubali ombi la Rais William Ruto la kusitisha maandamano ya Azimio kote nchini. Rais alisema yuko tayari kushirikisha upinzani kwa njia ya pande mbili kutafuta suluhu.

Chanzo: Radio Jambo