Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya: Deni kumpeleka rais Ruto China

Kenya: Ruto Afanya Mabadiliko Katika Baraza La Mawaziri Kenya: Deni kumpeleka rais Ruto China

Fri, 6 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Kenya, William Ruto anatarajiwa kufanya ziara nchini China baadae mwezi huu akiwa na lengo kutafuta mkopo wa Dola bilioni moja kufadhili miradi iliyokwama, naibu wa rais Rigathi Gachagua amethibitisha.

Akizungumza na kituo cha redio cha Inooro kinachotagaza kwa lugha ya mama, naibu rais amesema wanakandarasi katika baadhi ya maeneo kwenye taifa hilo wamesusia kazi kwa kukosa kulipwa kutokana na kazi wanayofanya.

Gachagua amesema kuwa licha ya kwamba Kenya inadaiwa na China, rais Ruto anatafuta mkopo zaidi wa Dola bilioni moja pamoja na kutafuta namna ya kulipia deni ambalo China inadai nchi yake.

Kenya inadaiwa na China zaidi ya Dola bilioni 8 kutokana na mikopo inayodaiwa kutolewa wakati wa serikali ya zamani chini ya rais Uhuru Kenyatta kwa ajili ya miradi ya miundombinu.

Naibu rais alizungumzia swala la ubadhirifu unaofanywa na maafisa wa serikali akisema hilo ndilo limesababisha rais kuagiza kuzuiliwa kwa safari za nje za maofisa wa serikali.

Mapema wiki hii, ofisi ya rais ilipiga marufuku maafisa wa umma kufanya safari zisizo za lazima nje ya nchi ili kubana matumizi na imeziagiza wizara zote kupunguza bajeti ya mwaka ujao wa fedha kwa asilimia 10.

Serikali imeshutumiwa kwa matumizi yasiyo ya lazima wakati huu raia wa taifa hilo wakikerwa kutokana na kupanda kwa gharama ya maisha na nyongeza ya ushuru iliyotangazwa na serikali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live