Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya,China na njia ya reli isiyokwenda popote

Reli China Kenyaaaa.jpeg Kenya,China na njia ya reli isiyokwenda popote

Sun, 15 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Sehemu ya kwanza ya reli ya Kenya iliyojengwa na China ilifunguliwa kwa shangwe mwaka 2017 - lakini miaka miwili baadaye kazi ya reli hiyo ilisimama katikati ya nchi na mpango mkuu wa kuiunganisha na nchi nyingine zisizo na bandari katika Afrika Mashariki unaonekana kuvurugika. Hii inamaanisha kuwa mradi huo hauleti pesa nyingi kama ilivyotarajiwa wakati huu, huku Kenya ikisalia kulipa mikopo ya jumla ya $4.7bn (£3.9bn), hasa iliyokopwa kutoka kwa benki za China. Hata hivyo ni vigumu kuamini kwamba Reli ya Standard Gauge ya Kenya (SGR) haijafaulu wakati abiria wanapotoka kwenye treni iliyojaa ya takriban mabehewa 12 kwenye kituo cha reli ya Syokimau katika mji mkuu, Nairobi - huduma ya mwisho kwa siku hiyo. Wamesafiri bila kusimama kutoka mji wa bandari wa Mombasa, umbali wa kilomita 470 (maili 290) kwenye Bahari ya Hindi. "Ni vizuri," msafiri Pauline Echesa mwenye umri wa miaka 53 aliniambia. Safari ya saa nne na nusu inampa bonasi ya kutazama wanyamapori njiani wakati reli inapita kwenye mbuga za kitaifa, anasema. CHANZO CHA PICHA, AFP Maelezo ya picha, Baadhi ya abiria wanaweza kufurahia wanyamapori kwenye Madaraka Express, ambayo hupitia mbuga za kitaifa Msafiri mwenye umri wa miaka 30 anasema safari ilikuwa ya kuchosha zaidi, akisema viti havikuwa vya kustarehesha lakini safari hiyo iliokoa pesa zake ikilinganishwa na njia zingine za kusafiri kutoka pwani. Hakuna shaka upande wa biashara ya abiria unafanya vizuri na umehifadhiwa kikamilifu, lakini hauwezi kulipa mikopo yenyewe - na haikukusudiwa kufanya hivyo. Mzigo huu unaangukia upande wa shehena ya biashara - kuleta ndani kontena zinazofika bandari ya Mombasa. Ilikusudiwa zifike Uganda, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Tatizo ni kwamba zinaweza kwenda tu hadi mji wa Naivasha nchini Kenya - kilomita 120 kutoka Nairobi lakini bado mbali na mpaka wa Uganda - kwenye SGR. Treni nyingi za mizigo kisha hurudi Mombasa zikiwa bure, hasara kubwa ya mapato. "Itakuwa na tija zaidi kwetu kuendelea na mradi," Waziri wa Uchukuzi wa Kenya Kipchumba Murkomen aliambia BBC. "Lakini sehemu ya ufadhili ni changamoto yetu." Anasema serikali itakuwa ikichunguza njia za kufadhili ujenzi wa sehemu iliyobaki ya reli wakati wa Mkutano ujao wa Ukanda na Barabara nchini China. Ulizinduliwa mwaka wa 2013, Mpango mkubwa wa China wa Belt and Road Initiative (BRI) umeenea kote ulimwenguni na kubadilisha kwa kiasi kikubwa mandhari ya miundombinu barani Afrika. Lakini mustakabali wake ni suala la mjadala sasa wakati China ikiendelea kupunguza ufadhili na nchi za Afrika zinakabiliwa na ukweli wa kuongezeka kwa madeni ambayo katika baadhi ya matukio yanatishia kuyumbisha uchumi wao. Baraza la Mahusiano ya Kigeni la Marekani linasema kuwa baadhi ya uwekezaji wa BRI umehusisha michakato ya zabuni isiyoeleweka na kuhitaji matumizi ya makampuni ya Kichina na kusababisha gharama za kupanda ambazo katika baadhi ya kesi zimesababisha kufutwa kwa miradi na upinzani wa kisiasa. Masuala ya ndani ambayo yameathiri uchumi wa China pia yamesababisha kupungua kwa ufadhili, anasema Naibu Gavana wa zamani wa Benki Kuu ya Nigeria, Kingsley Moghalu. "Ngazi za ufadhili katika miaka michache iliyopita hazijakuwa zaidi ya $2bn katika bara zima," anasema - chini, anakadiria, kutoka kati ya $10bn na $20bn muongo mmoja uliopita. SGR ya Kenya ni mojawapo ya zilizoathirika. CHANZO CHA PICHA, REUTERS Maelezo ya picha, Kenya inatarajia kupata msaada wa kujenga njia ya SGR hadi mpaka wa Uganda kwenye Mkutano wa Ukanda na Barabara nchini China. Lakini Bw Murkomen anasema Kenya iko wazi kwa chaguo: "Tuna wadau wa sekta ya kibinafsi nchini China ambao wamesema wako tayari kuweka rasilimali zao katika mradi na tunaweza kuwa na mazungumzo kuhusu jinsi watakavyorudisha fedha zao." Moja inaweza kuwa kipindi cha afueni kuruhusu nchi kwanza kulipa mikopo iliyochukuliwa ili kufadhili sehemu za reli ambazo zimekamilika, anaelezea. Hatua ya kukiri kwamba serikali inatafuta ufadhili zaidi huenda isiwapendeze wengi nchini ambao tayari wameyumba kutokana na nyongeza ya ushuru iliyoletwa na Rais William Ruto tangu aingie afisini mwaka mmoja uliopita. Wakenya wana wasiwasi kuwa ulipaji wa deni unaleta shinikizo kubwa kwa uchumi wa nchi. Takwimu za serikali kuanzia mwisho wa Juni 2022 zilionyesha kuwa Uchina ilikuwa mkopeshaji mkuu wa tatu wa nje wa Kenya - ikichukua 19.4% ya deni la nchi. "Kwa sasa, hali ya deni la nchi ni kubwa sana," anasema mwanauchumi wa Kenya Ken Gichinga, akielezea kuwa Juni ijayo ndipo Kenya italazimika kulipa $2bn ya Eurobond. “Na pia kuna hisia kwamba si pesa zote hizo zilitumika kujenga reli hiyo,” asema Bw Gichinga. Kukosekana kwa uwazi katika mikataba ambayo nchi kama Kenya imetia saini na Uchina ni suala la wasiwasi kwa raia wao wenyewe na wakosoaji wa nje ya nchi. Tathmini ya Baraza la Mahusiano ya Kigeni inabainisha kuwa masharti ya mkopo hayawekwi hadharani na "kwa sababu Uchina ilikataa kujiunga na Klabu ya Paris ya wadai wakuu rasmi", benki za Uchina hazina shinikizo la kupunguza viwango vya mikopo au kushiriki maelezo. Hii, inamaanisha hatari kwa Marekani na nchi zinazopokea "zilizidi faida zake". CHANZO CHA PICHA, AFP Ili reli ya Kenya ivune manufaa ambayo iliazimia wakati wa kuanzishwa kwake, inahitaji kwenda kimataifa. "Uganda pia inahitaji kuwa ndani," anasema Bw Gichinga. Lakini tamaa hiyo inaonekana kutetereka. Mpango Mkuu wa awali wa Usafiri wa Afrika Mashariki, uliopendekezwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki karibu miongo miwili iliyopita, ulitaka njia mbili katika nchi zisizo na bandari kutoka pwani - moja ikitoka Kenya, inayojulikana kama ukanda wa kaskazini, na nyingine kutoka Tanzania, iliyopewa jina la ukanda wa kati. Wakati huo ilikuwa na uhusiano na Sudan Kusini na DR Congo. Hata hivyo Uganda inaweza kuamua kusukuma biashara yake kuelekea Tanzania. Mradi wake wa reli umegharimu kiasi kidogo zaidi cha fedha kujenga na unatoa kasi ya juu kwani njia hiyo ina umeme. Rais wa zamani wa Tanzania John Magufuli alivunja makubaliano ambayo yalitiwa saini na mtangulizi wake na China kujenga reli hiyo na kuchagua kupata ufadhili badala yake kutoka Uturuki na Ureno kufadhili hatua ya kwanza ya mradi huo. Tanzania pia inaonekana kwenye njia ya kuungana na Rwanda, Burundi na DR Congo - huku China ikiingia katika sehemu za mwisho. Bw Moghalu anahoji kuwa, kama Tanzania, nchi katika bara "zinapaswa kuwa madereva wa hatima yao". "Nchi za Kiafrika zinahitaji kurekebishwa kiakili na kutojisikia kama wenzi walionyanyaswa na kwamba wanapaswa kuishukuru China kwa sababu wenzi wao wa zamani, Magharibi, hawakuwatendea vyema." Nchi za Magharibi hivi karibuni zimekuwa zikijaribu kukabiliana na BRI, ikiwa ni pamoja na Mpango wa Rais wa Marekani Joe Biden wa Build Back Better World Initiative, uliozinduliwa mwaka 2021 kwa ushirikiano na uchumi wa G7. Lakini kuna makubaliano ya ujumla kwamba China bado inaweza kutoa zaidi katika suala la maendeleo ya muda mrefu. Kwa wasafiri wa Nairobi-Mombasa, uwekezaji kama huo kwa mustakabali wa nchi ni wa manufaa. "Wacha tujitoe dhabihu ili kulipa deni na kupata zaidi kwa miradi kama hiyo," Bi Echesa aliambia BBC. Serikali ya Kenya itakuwa na matumaini kuwa inaweza kushawishi Uchina, na benki zake, kwamba reli ya SGR itakuwa na faida ikiwa itafika mpakani na kwingineko.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live