Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya: Aliyenaswa na mafuriko aokolewa kutumia helikopta

Mafuriko Kenya Kenya: Aliyenaswa na mafuriko aokolewa kutumia helikopta

Wed, 24 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mvulana aliyekuwa peke yake mwenye umri wa miaka mitano ambaye alikuwa amezingirwa na mafuriko Jumanne aliokolewa na helikopta ya polisi huko Yatta, yapata kilomita 120 kutoka mji mkuu wa Kenya, Nairobi.

Mvulana huyo "alikuwa ameachwa nyuma na babake wakati kina cha maji kilipoanza kupanda," polisi walisema.

Shiriki la Kimataifa lisilo la serikali la Masuala ya Kibinadamu, ambalo lilinasa eneo alilokuwa mvulana huyo kwa kutumia ndege zisizo na rubani, liliwaarifu polisi, ambao kisha walituma helikopta ya uokoaji kutoka Nairobi.

Jaribio la awali la kumwokoa mtoto huyo kwa boti lilishindikana kutokana na hali mbaya ya hewa, Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya lilisema.

"Mtoto huyo, ambaye alionekana kuwa na hofu baada ya kukwama kwa muda mrefu, aliokolewa salama na kupelekwa hospitali ya karibu kwa huduma," iliongeza.

Mvua kubwa zimekuwa zikinyesha nchini Kenya na Afrika Mashariki katika siku za hivi karibuni na kusababisha mafuriko na uharibifu mkubwa.

Nchini Kenya, mafuriko yamerekodiwa katika kaunti 23 kati ya 47 za nchi hiyo.

Zaidi ya watu 188 wameokolewa tangu kuanza kwa mafuriko yanayoendelea, Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya lilisema Jumanne.

Iliongeza kuwa mafuriko hayo yamesababisha kaya 11,206 kupoteza makazi, kuzamisha ekari 27,716 na kuua zaidi ya mifugo 4,800.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live