Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya Airways Kutaifishwa na Serikali, Kupunguza Wafanyakazi

Kenya Airways Flight Kenya Airways Kutaifishwa na Serikali, Kupunguza Wafanyakazi

Tue, 7 Jul 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la ndege la Kenya (Kenya Airways) limeanza mchakato wa miezi mitatu wa kupunguza wafanyakazi wakati ambao wabunge wa taifa hilo wanaandaa sheria itakayotaifisha shirika hilo na kumilikiwa na serikali kutokana na athari zitokanazo na janga la virusi vya Corona.

Mchakato huo wa kumilikiwa na serikali unatarajiwa kukamilika ifikapo Septemba 30 kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu, Allan Kilavuka katika taarifa alitotoa kwa wafanyakazi wa shirika hilo, kwa mujibu wa Bloomberg.

Taarifa hiyo kwa wafanyakazi inatabiria kupungua kwa mahitaji ya usafiri wa anga baada ya shughuli kurudi kutokana na wasafiri kusita kuendelea na maisha kama kawaida.

‘’Tumefanya makadirio kuwa mahitaji yataanguka kwa angalau 50% kati ya sasa hadi Disemba. Mali zetu zinapaswa kuangazia hilo. Shughuli zetu zinapaswa kuakisi hilo, bila hata kusema'', Kilavuka anasema.

Taarifa ya Bloomberg inasema kwamba Kenya Airways ilikuwa ina wafanyakazi 3,734 kufikia mwaka 2019 ikiwa inalipa mishahara inayofikia dola milioni 126.6. Hiyo ni wala 11% ya gharama za uendeshaji wa shirika hilo kwa mwaka. Ndege za abiria zinachangia wastani wa 81% ya mapato ya Kenya Airways kufikia 2019, huku ndege za mizigo zikichangia 8.1% tu ya mapato.

Mapema wiki hii, Jumuiya ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga (IATA) ilizitaka serikali za kiafrika kuangazia upya mahitaji ya karantini ya lazima kwa wasafiri wanaoingia barani Afrika ili kuruhusu uchumi kufufuka.

IATA inasema kuwa 80% ya wasafiri hawapo tayari kusafiri kwenda katika nchi ambazo watakaa karantini kwa wiki mbili, wakiongeza kuwa matokeo ya hatua hizi yanamaanisha kuwa nchi zitabaki kujifungia hata pale mipaka itakapokuwa wazi.

Taasisi hilo imeonya kuwa zaidi ya ajira milioni 8.6 barani Afrika na Mashariki ya kati kwenye sekta zinazotegemea usafiri wa anga zipo katika hatari ya kupotea kutokana na kuwepo kwa nchi kujifungia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live