Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya: Afisa wa polisi auawa na wenzake baada ya kumpiga risasi hakimu

Kortini Geita.jpeg Kenya: Afisa wa polisi auawa na wenzake baada ya kumpiga risasi hakimu

Thu, 13 Jun 2024 Chanzo: Bbc

Afisa wa polisi ameripotiwa kumpiga risasi na kumjeruhi hakimu mwandamizi katika Mahakama ya Makadara jijini Nairobi, Ofisi ya msajili mkuu wa mahakama imesema.

Polisi huyo anasemekana kumpiga risasi hakimu wakati akiwa anatoa uamuzi wa kesi inayomhusisha mke wake.

‘’Tunasikitika kuripoti tukio la kupigwa risas lenye kumhusisha afisa wa polisi na Hakimu katika Mahakama ya Makadara mnamo tarehe 13 Juni 2024,’’ Ofisi ya msajili mkuu wa mahakama ilisema.

Wakati kikao cha wazi cha mahakama kinaendelea, hakimu alifuta dhamana kwa mshtakiwa ambaye alikosa kufika mahakamani baada ya kupewa dhamana na kushindwa kutoa maelezo ya kuridhisha kwanini alifanya hivyo.

Ofisi ya msajili mkuu wa mahakama imesema, ‘mara baada ya uamuzi huo kutolewa mtu alimpiga risasi hakimu na kumjeruhi kwenye nyonga’.

Maafisa wa polisi waliokuwepo eneo la tukio walijibu haraka kwa kumpiga risasi na kumuua huku hakimu akikimbizwa hospitali kwa matibabu.

Chanzo: Bbc