Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kenya: 76 hawajulikani waliko baada ya mafuriko kusomba nyumba zao

Kenya: 76 Hawajulikani Waliko Baada Ya Mafuriko Kusomba Nyumba Zao Kenya: 76 hawajulikani waliko baada ya mafuriko kusomba nyumba zao

Tue, 30 Apr 2024 Chanzo: Bbc

Takriban watu 76 hawajulikani waliko nchini Kenya huku kukiwa na mafuriko makubwa ambayo tayari yamesababisha maafaya makumi ya watu, Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya linasema.

Watu katika vijiji karibu na Mai Mahiu, yapata kilomita 60 kutoka mji mkuu, Nairobi, walisombwa na maji walipokuwa wamelala Jumatatu asubuhi.

Kisa hicho kilitokea baada ya maji kuvuma kwenye mtaro ulioziba chini ya njia ya reli.

Takriban watu 50 walikuwa wamethibitishwa kufariki kufikia Jumatatu jioni, huku Shirika la Msalaba Mwekundu likiongeza Jumanne kwamba manusura 110 wameokolewa.

Kwa siku ya pili, waokoaji wanajaribu kuokoa wale ambao wamenaswa chini ya vifusi. Pia wanajaribu kuopoa maiti kutoka kwenye matope huku kukiwa na hofu kwamba idadi ya waliofariki inaweza kuongezeka zaidi.

"Ninajaribu kuokoa vitu vilivyochukuliwa na maji na kutafuta watu waliopotea pia," Stephen Kamau, mwanakijiji ambaye aliponea chupuchupu katika maafa hayo, aliambia BBC.

"Niliamka katika ulimwengu tofauti. Kila kitu kilikuwa kimesombwa na maji. Tuna hofu. Moyo wangu ni mzito."

Maafisa kutokaHudumaya vijana wanaotumikia Taifa (NYS) wameungana na wenyeji na Shirika la Msalaba Mwekundu katika juhudi zao za kutafuta manusura.

Kwa jumla, karibu Wakenya 170 wameuawa katika mvua kubwa na mafuriko katika muda wa mwezi mmoja uliopita.

Chanzo: Bbc