Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kazungu jela maisha kwa mauaji ya watu 14

Denis Kazungu Ew Kazungu jela maisha kwa mauaji ya watu 14

Mon, 11 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya jijini Kigali imemuhukumu raia wake Denis Kazungu, kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya mauaji ya watu kadhaa, ambao miili yao ilikutwa imezikwa nyumbani kwake.

Kazungu alikamatwa Septemba 2023, baada ya Polisi kufanya msako nyumbani kwake jijini Kigali na kugundua miili ya watu hao.

Kuhukumiwa kwake kunafustia ushahidi ulikutwa nyumbani kwake na pia alikiri kuwauwa Wanawake 13 na Mwanaume mmoja, akidai walimuambukizwa virusi vya Ukimwi.

Aidha, Kazungu alipokamatwa, alisema aliwarubuni watu hao na kwenda nao nyumbani kwake, kisha kuwabaka, kuwaibia na kuwaua.

Septemba 21, 2023, Kazungu alikiri makosa ya mauaji hayo na alihukumiwa kifungo cha maisha jela Machi 8, 2024.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live