Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kaya maskini kuanza kulipwa Nigeria

Naira Kaya maskini kuanza kulipwa Nigeria

Fri, 14 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

RAIS mpya wa Nigeria Bola Tinubu ametangaza mpango wa serikali yake kutoa dola 10 (Sh 24,000) kwa mwezi kwa kaya maskini ili kupunguza ugumu wa maisha unaosababishwa na kufutwa kwa ruzuku ya petroli. - Katika barua yake kwa Seneti ya Nigeria, ambayo ilisomwa wakati wa kikao cha Alhamisi, Tinubu alisema kaya milioni 12 zitafaidika na mpango huo kwa muda wa miezi sita. Serikali inapanga kuifadhili kupitia mkopo wa Benki ya Dunia wa dola milioni 800 ambao Tinubu anatafuta idhini ya wabunge. - "Inatarajiwa kuwa mpango huo utachochea shughuli za kiuchumi katika sekta isiyo rasmi na kuboresha lishe, afya, elimu, na maendeleo ya mtaji wa watu wa kaya za walengwa," alisema kuhusu mpango wa ustawi wa jamii.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live