Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kauli ya Jeshi Baada ya Kumpindua Rais Conde Guinea

Guinea 1 1?fit=800%2C450&ssl=1 Kauli ya Jeshi Baada ya Kumpindua Rais Conde Guinea

Mon, 6 Sep 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

UMOJA wa Afrika (AU) umelaani mapinduzi ya kijeshi nchini Guinea na kulitaka jeshi la nchi hiyo kumuachilia Rais Alpha Conde mara moja.

Katika taarifa Rais wa AU, Felix Tshisekedi na Rais wa Tume ya AU, Moussa Faki wameitisha mkutano wa dharura wa taasisi za umoja huo kuhusu Usalama na Amani ili kutathimini hali nchini Guinea na kuchukua hatua zifaazo.

Hapo jana katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Gutteres ametuma ujumbe wa twitter akijibu kinachotokea Guinea akisema kwamba anafuatilia hali hiyo kwa karibu na huku akilaani kupinduliwa kwa serikali kwa kutumia nguvu ya bunduki na akataka kuachiliwa mara moja kwa Rais Alpha Conde.

I am personally following the situation in Guinea very closely. I strongly condemn any takeover of the government by force of the gun and call for the immediate release of President Alpha Conde.

— António Guterres (@antonioguterres) September 5, 2021.

Hatima ya Rais wa Guinea, Alpha Condé haijulikani wazi baada ya video ambayo haijathibitishwa kumuonyesha mikononi mwa wanajeshi, ambao walisema wamefanya mapinduzi.



Waziri wa ulinzi amenukuliwa akisema jaribio la kuichukua serikali lilikuwa limeshindwa. Hii inafuatia masaa mengi ya makabiliano ya risasi karibu na ikulu ya rais katika Mji Mkuu, Conakry.

Jeshi ambalo limedai kuchukua madaraka nchini humo limetangaza kwamba litafanya mkutano leo na mawaziri na wakuu wa taasisi zilizovunjwa jana Mjini Conakry. Wanajeshi hao pia wametangaza amri ya kutotoka nje kuanzia saa mbili usiku.

Bado haijulikani ni nini kinatokea huko Conakry, lakini wanajeshi wanasema wamechukua udhibiti. Katika hotuba iliyoonyeshwa kwa njia ya televisheni, wanaume walio na sare za kijeshi, bendera ya Guinea ikiwa nyuma yao wamelihutubia taifa.

Wakijiita Kamati ya Kitaifa ya upatanisho na maendeleo, wanalaumu ufisadi uliokithiri, usimamizi mbaya na umasikini nchini Guinea kwa uamuzi wao wa kufanya mapinduzi. Wanasema katiba imevunjwa na kwamba kutakuwa na mashauriano ya kuunda katiba mpya, inayowahusisha watu wote.

Wamedai pia kwamba serikali imevunjwa na kwamba mipaka ya ardhi itafungwa kwa wiki moja. Katika picha na video zilizowekwa katika mitandao ya kijamii, mtu ambaye anaonekana kuwa rais Alpha Condé, amevaa mavazi ya kawaida na shati iliyochapishwa maua anaonyeshwa akiwa amekasirika akiwa amezungukwa na wanaume walio na sare za jeshi.

Katika video moja, ameulizwa kwa Kifaransa ikiwa ameumizwa kwa njia yoyote lakini hajibu. Ubalozi wa Australia umewauliza raia wake kukaa mahali salama na kutazama vyombo vya habari vya ndani na taarifa kutoka kwa balozi.



Kumekuwa na ripoti nyingi za milio ya risasi katika mji mkuu wa nchi hiyo ya Afrika Magharibi jana Jumapili asubuhi. Wakazi wa eneo hilo wameambia mashirika ya habari kuwa wanajeshi wamekuwa wakifanya doria mitaani na wamefunga daraja kuelekea mtaa ambao Ikulu ya rais iko. Wakazi wenye hofu ya wilaya kuu ya Kaloum wametii maagizo yao ya kukaa nyumbani.

Daraja la pekee linalounganisha bara na eneo la Kaloum, ambalo lina wizara nyingi na Ikulu ya rais, lilikuwa limefungwa na wanajeshi wengi, wengine wakiwa na silaha nzito, walikuwa wamezunguka Ikulu, chanzo cha jeshi kiliambia Reuters.

Video zilizowekwa kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha misafara ya magari ya kubeba silaha na malori yanayobeba askari wanaofanya doria mitaani, ingawa hizi hazijathibitishwa.

Rais Conde alichaguliwa kwa muhula wa tatu uliokumba na utata ambao ulisababisha ghasia mwaka jana .Mwanasiasa huyo mkongwe alichaguliwa mara ya kwanza kuwa rais mwaka wa 2010 katika uchaguzi wa kwanza ulioshuhudia makabidhiano ya mamlaka ya njia ya Amani.

Licha ya utawala wake kufanikiwa kuboresha hali ya uchumi amelaumiwa kwa kuongoza serikali inayokiuka haki za binadamu na unyanyasaji wa wakosoaji wake .

Chanzo: globalpublishers.co.tz