Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Katumbia asije kuwa kama George Weah

Moses Katumbi.jpeg Katumbia asije kuwa kama George Weah

Tue, 26 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanafamilia wa mpira wa miguu, George Weah hivi karibuni katema bungo huko kwao Liberia baada ya kupigwa chini katika kinyang’anyiro cha kuwania Urais wa nchi hiyo katika Uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo uliofanyika Oktoba 10 mwaka huu.

Ameangushwa na makamu wa zamani wa Rais wa nchi hiyo Joseph Boakai ambaye amepata asilimia 50.64 ya kura zote zilizopigwa huku George Weah akiwa amepata kura asilimia 49.36.

Weah ameanguka katika uchaguzi huo huku akiwa ndio Rais aliyekuwa madarakani ambapo aliitumikia nafasi hiyo kwa miaka sita tangu 2017 alipomuondoa madarakani aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Ellen Johnson-Sirleaf.

Kwa walio nje ya Liberia wameshangazwa kwa Weah ambaye alikuwa mwanasoka maarufu miaka ya nyuma akizichezea AC Milan, Monaco, PSG, Manchester City na Chelsea kushindwa uchaguzi huo lakini kwa raia wa nchi hiyo wala hawajaona kitu cha kushtua na wengi wamefurahia kumuangusha George Weah mbele ya Boakai.

Sababu iko wazi ambayo ni kushinda kutimiza matarajio ya raia wengi wa Liberia ambao walikuwa na matumaini naye kwamba ataiweka nchi hiyo kwenye mstari kwa kuimarisha uchumi na sekta nyinginezo pamoja na kupambana na changamoto kama vile rushwa na matumizi mabaya ya rasilimali za serikali.

Matokeo yake yalikuwa kinyume ambapo ilishuhudiwa yale ambayo wananchi wa Liberia walitegemewa yangeshughulikiwa na kupunguzwa au kumalizwa na Weah ndio yakaongezeka na hali ya nchi yao ikazidi kuwa mbaya.

Nimekumbuka hadithi ya Weah baada ya kusikia mmiliki wa TP Mazembe, Moise Katumbi ni miongoni mwa watu waliojitokeza kuwania nafasi ya Urais wa DR Congo mwingine akiwa ni Rais anayemaliza muda wake, Felix Tsishekedi wakiwa ndio wagombea wanaopewa nafasi kubwa.

Inawezekana tajiri Moise Katumbi safari hii akatimiza ndoto yake ya muda mrefu kupitia uchaguzi huu wa sasa lakini pia hilo linaweza kutotimia iwapo raia wa DR Congo wataamua kumchagua mgombea mwingine.

Kama akiibuka mshindi, Katumbi anapaswa kuhakikisha anapigania maisha ya raia wake na kuhakikisha yanakuwa bora na kuepuka ubadhilifu ili asije kufuata nyayo za mtu mwenzake wa mpira George Weah.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live