Tajiri wa timu ya TP Mazembe, Moise Katumbi yamemkuta mapya baada ya kuzuiwa kusafiri kwenda kutazama dabi ya kati ya timu yake na FC Lupopo inayopigwa leo.
Muda mfupi ujao Mazembe itashuka uwanjani kumenyana na Lupopo mechi itakayochezwa Jiji la Kalemie ukihamishwa kutoka Lubumbashi ikihofiwa kuwepo na ghasia kutokana na upinzani wa timu hizo mbili.
Katumbi ambaye ni mmoja wa wagombea wa uchaguzi mkuu wa nchi hiyo amefika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Lubumbashi maarufu kwa Luano tayari kwa safari na kukutana na zuio hilo.
Bilionea huyo amekutana na taarifa ya mamlaka ya anga kuwa ndege yake binafsi imekosa kibali cha kutua Jiji la Kalemie hatua ambayo itamfanya kuikosa mechi hiyo.
Inaelezwa zuio hilo liachangiwa na kuhofiwa machafuko yanazoweza kutokea baina ya mashabiki wa klabu hizo mbili kulikuwa na kila dalili za Katumbi kuzuiwa kwenda Jiji la Kalemie kutokana na mgombea huyo kuanza kulalamikia mchakato wa uchaguzi wa urais ambao matokeo ya jumla yatatangazwa kesho Jumapili.
Mapema wiki hii Katumbi amesikika akikosoa mchakato wa uchaguzi uliofanyika nchini humo akidai mambo mengi hayakwenda kwa usawa katika kuondoa udanganyifu wa matokeo hayo ambayo mpaka jana mpinzani wake mkubwa Felix Tshekedi alikiuwa anaongoza kwa zaidi ya asilimia 70.