Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Katumbi amkacha Rais Tshisekedi

09625fc6cc34690f508f5193ab73d719 Katumbi amkacha Rais Tshisekedi

Fri, 22 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

CHAMA cha Ensemble pour la Republique kinachoongozwa na mfanyabiashara maarufu wa nchini Congo DRC, Moise Katumbi kimetangaza kujitoa kwenye muungano mpya wa 'Union Sacree', ulioundwa na Rais wa nchi hiyo Felix Tshisekedi.

Akitangaza taarifa ya chama hicho kujitoa kwenye umoja huo, Mbunge Muhindo Nzangi ambaye pia ni msemaji wa chama hicho alisema wameamua chama chao kuendelea kubaki upande wa upinzani.

''Ujumbe tulio nao leo ni kwamba mazingira yaliopo hivi sasa hayaturuhusu kuendelea kubaki ndani ya muungano wa Union sacrée.” amesema Nzangi na kuongeza:

“Ujumbe wa wazi uliotumwa na wenzetu waliopo na Rais Tshisekedi ni kwamba tuliwasaidia kumuondoa Spika wa bunge kutoka chama cha FCC cha Joseph Kabila, lakini wataendelea kushirikiana na wabunge kutoka chama hicho.''

Chama cha Katumbi kimeelezea kwamba Rais Tshisekedi anadhamiria kuteuwa Waziri Mkuu mpya ambaye ni kutoka miongoni mwa wabunge waliokihama chama cha FCC cha Kabila. Na vilevile anatarajia kuunga mkono spika mpya wa bunge kutokana na vuguvugu hilo la FCC.

Taarifa kutoka Ikulu ya Rais Tshisekedi pia zinasema kwamba vyama vya Katumbi na Bemba viliomba kupewa nyazifa za waziri mkuu na spika wa bunge.

Hata hivyo, Msemaji wa chama cha UDPS cha Tshisekedi amesema kwamba mazungumzo yanaendelea baina ya rais na viongozi hao wawili wa upinzani, ili kumaliza tofauti zao.

Chanzo: habarileo.co.tz