Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Katibu wa kudumu Magereza Kenya ajiuzulu baada ya kuteuliwa

Katibu Wa Kudumu Magereza Kenya Ajiuzulu Baada Ya Kuteuliwa Katibu wa kudumu Magereza Kenya ajiuzulu baada ya kuteuliwa

Tue, 23 May 2023 Chanzo: Bbc

Katibu wa kudumu wa idara ya magereza nchini Kenya Esther Ngero amejiuzulu, vimeripoti vyombo vya habari nchini humo.

Hii ni mara ya kwanza kwa afisa wa cheo chake kujiuzulu, tangu Rais William ruto aingie mamlakani.

Rais William Ruto mnamo Jumanne alikiri kupokea kujiuzulu kwa Bi Ngero kupitia taarifa ya Mkuu wa Utumishi wa Umma Felix Koskei.

"Mheshimiwa Rais amepokea na kukubali kwa masikitiko kujiuzulu kwa Bi Esther Ngero, Katibu wa kudumu wa idara ya magereza, ambaye anaondoka ofisini kwa sababu za kibinafsi," ilisema taarifa hiyo.

Bi Ngero alipewa wadhifa huo mwezi tarehe 16 Mei falsemwaka huu.

Kabla ya kuingia serikalini akiwa Katibu mnamo Desemba 2022 baada ya kuteuliwa, Bi Ngeru alikuwa akifanya kazi katika sekta ya mafuta kwa miongo

Chanzo: Bbc