Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Katibu Mkuu UN ahimiza chanjo ya corona Afrika

Habarileo Tz 131274629 901898097221839 2540560004784086428 N 660x400 Katibu Mkuu UN ahimiza chanjo ya corona Afrika

Mon, 14 Dec 2020 Chanzo: millardayo.com

Katibu Mkuu Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres ametoa wito kuwa kusiwepo na upendeleo katika ugawaji wa chanjo ya virusi vya corona na kwamba kila nchi ina haki ya kupata chanjo hiyo zikiwemo nchi za Afrika.

Akizungumza kwa njia ya video kwenye mkutano na Umoja wa Afrika, Guterres amesema anaona utaifa ukipewa kipaumbele kwenye suala la chanjo huku nchi tajiri zikipewa nafasi kubwa kuliko maskini.

“Bidhaa ya umma inapatikana kwa watu wote, kila mahali duniani na hasa barani Afrika ambako kuna mahitaji makubwa ya kukabiliana ipasavyo na msukosuko huo” Guteres

Hivi karibuni shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International, lilifichua kuwa nchi tajiri duniani zimenunua chanjo mara tatu zaidi ya zinavyohitajika, jambo ambalo linaweza kuwakosesha chanjo mabilioni ya watu katika nchi masikini.

“SITAKI UJINGA, WAHUNI MTAJUA SITAKI UANAHARAMU” SIRRO AWA MBOGO

Chanzo: millardayo.com