Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Katibu Mkuu OPEC afariki Dunia akiwa na umri wa miaka 63

Mohamed Barkindo Opep Katibu Mkuu OPEC afariki Dunia akiwa na umri wa miaka 63

Fri, 8 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali Nigeria pamoja na shirika la kimataifa la nchi ambazo zinazlisha mafuta OPEC, wamedhibitisha na kutangaza kifo cha katibu mkuu wake Mohammad Barkindo kilichotokea Jumanne jioni mjini Abuja.

Wizara ya mafuta ya Nigeria imewaambia wanahabari kwamba Barkindo mwenye umri wa miaka 63 aliaga dunia muda mfupi baada ya kukutana na rais wa Nigeria Muhhamadu Buhari.

OPEC yenye makao yake makuu mjini Vienna imedhibitisha kifo hicho bila kutoa maelezo zaidi.

Kifo chake kimeshtua wadau wengi kwenye sekta ya mafuta ulimwenguni kote, Mohammad Barkindo ameaga dunia wakati akikaribia kukamilisha muhula wake wa pili hapo Julai 31, ameushikilia wadhifa huo kama katibu mkuu wa OPEC kwa miaka 6 tangu mwaka wa 2016 hadi mauti yalipomkuta.

Habari za kifo chake zilitolewa kwa mara ya kwanza kupitia ujumbe wa twitter na mkurugenzi wa shirika la kitaifa wa shirika la mafuta nchini Nigeria, Mele Kyari.

Taarifa ya OPEC imesema kwamba maneno yake ya mwisho kwa rafiki zake yalikuwa kwamba amefurahi kukamilisha muda wake kama katibu mkuu, na kwamba alifanya kila awezalo kulitumikia shirika hilo, huku pia akiwasifu waliofanya kazi naye.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live