Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Katibu Mkuu Jumuiya ya Madola alaani mauaji Nigeria

05d69b7cf9d5f525d07f7338ac7c8d21 Katibu Mkuu Jumuiya ya Madola alaani mauaji Nigeria

Thu, 22 Oct 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola, Patricia Scotland amelaani vurugu zinazoendelea nchini Nigeria na kutaka wote wanaohusika na vurugu hizo wawajibishwe.

Scotland amesema anafuatilia kwa karibu vurugu hizo zinazoendelea nchini humo dhidi ya waandamanaji katika jiji la kibishara la Lagos na maeneo mengine ya Nigeria.

“Haki ya kufanya maandamano ipo katika katiba ya nchi hiyo, hivyo inapaswa kulindwa na kuheshimiwa na watekelezaji wa vitendo hivyo vya kinyama wanapaswa kuwajibishwa kwa mujibu wa sheria” amesema Scotland.

Katibu Mkuu huyo ametaka uchunguzi usio na upendeleo ufanyike haraka na matokeo yake yatangazwe kwa haki.

Kutokana na vurugu hizo Shirika la Haki za Binadamu la Amnesty International limetoa ripoti kuwa watu wasiopungua 12 waliuawa na wanajeshi na polisi huko Lagos siku ya Jumanne.

Maandamano hayo yalianza wiki mbili iliyopita mara baada ya kitengo cha jeshi la polisi la nchi hiyo (SARS) kinachohusika na upambaji dhidi ya wizi wa kutumia silaha, ambacho kimekuwa kinashutumiwa kwa kuwaweka watu kizuizini kinyume cha sheria na kushambulia raia kwa risasi jambo lililomshawishi Rais Muhhamadu Buhari wa nchi hiyo mnamo Oktoba 11 kukivunja kikosi hicho.

Chanzo: habarileo.co.tz