Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Katiba ya Shirikisho la Somalia imeidhinishwa bungeni

Rais Wa Somalia Katiba ya Shirikisho la Somalia imeidhinishwa bungeni

Sun, 31 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katika hatua ya kihistoria, wajumbe wa mabunge yote mawili ya Bunge la Shirikisho la Somalia wamepiga kura kuidhinisha katiba ya shirikisho baada ya miaka mingi ya mijadala na ucheleweshaji.

Kikao cha bunge hilo Jumamosi kilihudhuriwa na wabunge 254 kutoka Baraza la Juu na Baraza la Wananchi.

Rais Hassan Sheikh Mohamud amewekeza juhudi kubwa katika kukamilisha na kutekeleza katiba ambayo imekabiliwa na upinzani.

Serikali ya eneo lenye mamlaka ya ndani la Puntland lilikataa mchakato huo na kuutaja kuwa wa upande mmoja, wakati marais wa zamani Mohamed Abdullahi Farmajo na Sharif Sheikh Ahmed wameelezea wasiwasi wao juu ya kukosekana maelewano.

Eneo la Somaliland limejitangazia uhuru wake na halikushiriki katika mchakato huo.

Licha ya kuidhinishwa na bunge, katiba bado inahitaji kura ya maoni ya umma kukamilisha mpito wa Somalia hadi demokrasia ya kudumu ya kikatiba, kazi muhimu inayoisubiri serikali ya Mohamud.

Kura hiyo inaashiria hatua muhimu lakini changamoto zimesalia katika kuunganisha taifa hilo la Pembe ya Afrika kwa msingi wa katiba.

Somalia bado inakabiliwa na changamoto kubwa ya ugaidi ambapo magaidi wa Al Shabab hutekeleza mashambulizi ya mara kwa mara nchini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live