Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Katanga, Lubaga waachiwa huru Congo

99436 Pic+congo Katanga, Lubaga waachiwa huru Congo

Thu, 19 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kinshasa, DRC. Waliokuwa wafungwa wa kivita nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), Thomas Lubanga na Germain Katanga wameachiwa huru kutoka jela baada ya kumaliza kifungo chao.

Lubanga aliachiwa huru baada kutumikia kifungo cha miaka 14 jela wakati Katanga alikaa gerezani kwa miaka 12.

Waasi hao walihukumiwa na Mahakama ya Kimataifa ya uhalifu wa kivita (ICC) iliyopo mjini The Hague, Uholanzi.

Wafungwa hao wameachiwa huru wakati ambako machafuko yamezuuka upya nchini humo katika Mkoa wa Ituri.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa (UN), watu zaidi ya 700 wameuawa huku maelfu wakikimbia makazi yao kutokana na machafuko hayo.

Katanga na Lubanga walihamishwa kutoka The Hague, Uholanzi mwaka2015 na kupelekwa nchini Congo Kinshasa ambako walitumikia muda uliobaki wa kifungo.

Pia Soma

Advertisement
Kiongozi wa Shirika la kutetea za binadamu amani la ASADHO, Jean Katende alisema kurudi kwa viongozi hao kutachangia kurejesha amani katika eneo hilo la Ituri.

“Napenda kuona msimamo watakaokuwa nao baada ya kuachiwa huru, mchango wao kwa ajili ya amani na salama katika eneo hili ni muhimu sana.”

Mwaka 2003, Lubanga alipatikana na makosa ya kuajiri watoto wadogo katika kundi lake la waasi na kusababisha mauaji na vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu wakati Katanga aliongoza  kundi lililofanya mauaji ya zaidi ya watu 2000, katika Wilaya ya Ituri, Mashariki mwa Congo.

Chanzo: mwananchi.co.tz