Fri, 27 Aug 2021
Chanzo: Jamii Forums
Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema utoaji Chanjo dhidi ya #COVID19 Barani Afrika umeongezeka ikielezwa dozi Milioni 13 zilitolewa wiki iliyopita. Idadi hiyo ni mara tatu zaidi ya Chanjo zilizotolewa wiki ya kabla.
Mkurugenzi wa WHO Afrika, Matshidiso Moeti amesema Visa vipya 248,000 viliripotiwa wiki iliyopita huku angalau Nchi 28 zikikabiliwa na ongezeko la maambukizi kutokana na Kirusi cha Delta
Moeti amesema Afrika itapokea dozi Milioni 117 za Chanjo miezi ijayo, lakini Chanjo Milioni 34 za ziada zinahitajika ili kufikia lengo la kuwachanja 10% ya watu.
Chanzo: Jamii Forums