Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kashfa ya kuficha mamilioni ya fedha shambani kwa inayomkabili Rais Ramaphosa

Rais Ramaphosa 2.jpeg Rais Ramaphosa

Sun, 4 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kashfa ya Ramaphosa: Ilikuaje hadi zaid ya dola laki tano zikakutwa kwenye kochi?

Ripoti mbaya kutoka kwa jopo la watalaamu wa sheria inayodai kwamba rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa alificha wizi wa $4m (£3.3m) pesa taslimu katika shamba lake mwaka 2020 imezua maswali kadhaa kuhusu kiongozi huyo wa Afrika Kusini.

Jopo hilo linaloongozwa na aliyekuwa mwanasheria mkuu – liliezea baadhi ya maelezo yake ‘sio ya kweli’.

Bwana Ramaphosa ana kesi ya kujibu , sio tu mbele ya bunge bali pia kwa raia wa Afrika Kusini, wakosoaji wake wanasema

Kwa kuzingatia misimamo mikali ya vyama vya upinzani ambavyo baadhi yao vinamtaka aachie ngazi mara moja, kashfa hii ina uwezo wa kumgharimu kazi yake.

Katika wasilisho la kurasa 138 lililowasilishwa kwa jopo hilo, Rais Ramaphosa alikanusha kuwa kulikuwa na kitu kibaya kuhusu pesa zilizofichwa kwenye shamba lake la kibinafsi, akisema zilitokana na mapato ya nyati waliouzwa kwa dola 580,000 taslimu kwa raia wa Sudan, Mustafa Mohamed Ibrahim Hazim, mwishoni mwa 2019.

Hata hivyo, Bw Hazim hajajitokeza hadharani na ni machache yanayojulikana kumuhusu.

Jopo hilo lilihoji kwa nini stakhabadhi iliyowasilishwa kwao haikuwa na maelezo yoyote ambayo yangemfanya atambulike. Kulikuwa na jina lake tu, hakuna anwani ya biashara wala nambari ya kitambulisho.

Kwa heshima nasema mashtaka yote nilioitwa kuyajibu hayana msingi wowote , bwana Ramaphosa aliandika, akiongezea kwamba madai mengi yalikuwa uvumi . Aliomba kwamba suala hilo lisiendelezwe.

Lakini halijamuondokea na kuna shinikizo kwa rais kujiuzulu au ashtakiwe bungeni.

Ni vigumu kukosa kejeli ya madai na hali ambayo Rais huyo anijikuta.

Hii ni baada ya kiongozi huyo ambaye taswira yake ya kisiasa na kupanda madarakani hadi kuwa rais kulijengwa kutokana na vita vyake dhidi ya ufisadi, ambao ulitawala chama tawala cha African National Congress (ANC) na nchi nzima kwa ujumla chini ya mtangulizi wake Rais Jacob Zuma.

Wito wa Uchaguzi wa mapema Je, ni nini basi kifanyike kwa jinsi Bw Ramphosa alivyoshughulikia sakata ya "Farmgate"?

Chama chake kinajadili kwa ukali jinsi rais anapaswa kushughulikia ripoti hiyo, vyanzo vya chama vimesema.

Wakati wengine wanamtaka achukue mbinu ya kusubiri na kuona, wengine, kutoka kwa kundi pinzani la ANC, wanamtaka aondoke ili kuzuia uharibifu zaidi kwa chama, wanasema.

Ni rasmi, ofisi ya rais imesema ataishughulikia ripoti hiyo mara tu atakapomaliza kuisoma.

Bw Ramaphosa alifurahia neema fulani alipochukua mamlaka sio tu kutoka kwa umma lakini wafanyabiashara na mashirika ya kiraia - hata vyombo vya habari vya ndani kwa njia fulani.

Alitoa ahadi kubwa za mapambazuko mapya kwa Afrika Kusini chini ya uongozi wake na kuwasihi wananchi waamini kwamba anaweza kubadilisha mambo, kwamba siku za kashfa za ufisadi zingekuwa historia. Lakini neema hiyo sasa imepotea.

Upinzani mkuu nchini humo unasema kwamba kulingana na ripoti hii, rais ameonekana kuwa na kesi ya kujibu.

Chama cha Democratic Alliance kilitangaza kwamba kitatumia kikao cha bunge wiki ijayo kuwasilisha hoja ya kutaka uchaguzi wa mapema - kikisema shutma dhidi ya Bw Ramaphosa zinaonyesha kwamba ANC lazima iondolewe mamlakani.

"Ripoti iko wazi na haina utata. Rais Ramaphosa kuna uwezekano mkubwa alikiuka vifungu kadhaa vya Katiba na ana kesi ya kujibu. Taratibu za kumfungulia mashtaka ni lazima ziendelee, na atalazimika kutoa maelezo bora zaidi na ya kina kuliko alivyojielezea `hadi sasa," chama kilisema katika taarifa.

Ripoti hiyo iliyoundwa na juzuu tatu - inazua maswali kuhusu uwasilishaji wa maandishi wa Bw Ramaphosa:

Kwa nini rais alihifadhi dola 580,000 ndani ya sofa? Kwa nini wizi wa fedha hizo haukuripotiwa polisi miaka miwili iliyopita? Kwa nini nyati anaosema waliuzwa wanasalia kuwa shambani?

Katika maelezo ya Bw Ramaphosa, meneja wa nyumba ya kulala wageni katika shamba hilo kwanza alihifadhi pesa hizo kwenye sefu, lakini baadaye akazihamishia kwenye sofa katika chumba cha kulala cha ziada "ndani ya makazi yangu ya kibinafsi, kwa sababu alidhani kuwa ni mahali salama zaidi, kwani aliamini hakuna mtu angevunja na kuingia katika nyumba ya rais."

Jopo hilo liliamini kwamba maelezo yanahitaji kuchunguzwa zaidi.

Upeo wa majaji ulikuwa mdogo wa kupendekeza bunge kuchukua hatua.

Iwapo wabunge wataamua kwamba kamati ya kumuondoa rais ichunguze zaidi na kumpata rais na hatia ya utovu wa nidhamu, hilo lingeanzisha mchakato wa kura ya kumuondoa madarakani.

Hatimaye itafanyika kwa kura - hoja ya kumshtaki inahitaji kura ya thuluthi mbili bungeni ili kupitishwa.

Wakati ANC ina idadi ya kuzuia hilo kutokea, chama pia kimegawanyika pakubwa. Wanaompinga wanaweza kuona hii ni fursa ya kupiga kura na vyama vya upinzani kumuondoa.

Tumetoka kwa kura kama hiyo lakini katika mahakama ya maoni ya umma kile ambacho tayari kimeanzishwa kimemuharibia jina

Sifa mbaya kwa chama cha ANC' Vituo vya redio vya ndani na mitandao ya kijamii vimejawa na maoni tofauti kutoka kwa Waafrika Kusini - baadhi wanaamini analengwa na maadui zake wa kisiasa, huku wengine wakionyesha kusikitishwa na kutaka aondoke.

"Hii ni mbaya sana kwa ANC," mchambuzi wa kisiasa Oscar Van Heerden aliiambia Newzroom Afrika.

"Hakuna shirika linalotaka kiongozi anayehojiwa kwa namna hii. ANC inabidi ifikirie masuala ya kisiasa. Je, ni kwa manufaa yetu kumuondoa kiongozi wetu wakati huu? ANC inabidi ifanye uamuzi ambao utawaweka katika hali nzuri katika uchaguzi wa 2024."

Mkanganyiko huu unaweka msimamo wa maadili wa Bw Ramphosa katika maswali. Ubaya zaidi unaonyesha matumizi mabaya ya madaraka na pengine katiba - katiba ile ile aliyosaidia kuitayarisha mwanzoni mwa miaka ya 1990.

Chama chake, ambacho kimewatetea viongozi wake kupitia kashfa nyingi huko nyuma, kinalazimika kumfukuza tu ikiwa atapatikana na hatia.

Matukio haya yanajiri kabla ya kufanyika kwa kongamano la ANC mwezi huu, ambapo Bw Ramaphosa alionekana kuwa mwathirika wa kuchaguliwa tena kuwa kiongozi wa chama, yamemuweka mwanasiasa huyo mkongwe na mkulima katika hali mbaya.

Mambo saba kuhusu Cyril Ramaphosa:

Alizaliwa Soweto, Johannesburg, mwaka 1952

Alikamatwa mwaka wa 1974 na 1976 kwa shughuli za kupinga ubaguzi wa rangi na alizindua Muungano wa Kitaifa wa Wafanyakazi wa Migodini mwaka wa 1982.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Mapokezi iliyotayarisha kuachiliwa kwa Nelson Mandela kutoka gerezani mwaka 1990

Alikua mbunge na mwenyekiti wa bunge la katiba mwaka 1994

Aliingia katika biashara kwa muda wote mwaka wa 1997, na kuwa mmoja wa wafanyabiashara tajiri zaidi Afrika Kusini

Alikuwa kwenye bodi ya Lonmin wakati wa mauaji ya Marikana 2012

Alichaguliwa kuwa kiongozi wa ANC mwaka 2017 na tarehe 15 Februari 2018 akawa rais baada ya kujiuzulu kwa Jacob Zuma.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live