Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kashfa wizi wa mamilioni unavyotafuna Urais wa Ramphosa

RAMAPHOSA Kashfa wizi wa mamilioni unavyotafuna Urais wa Ramphosa

Fri, 2 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ripoti mbaya kutoka kwa jopo la watalaamu wa sheria inayodai kwamba rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa alificha wizi wa $4m (£3.3m) pesa taslimu katika shamba lake mwaka 2020 imezua maswali kadhaa kuhusu kiongozi huyo wa Afrika Kusini.

Jopo hilo linaloongozwa na aliyekuwa mwanasheria mkuu – liliezea baadhi ya maelezo yake ‘sio ya kweli’.

Bwana Ramaphosa ana kesi ya kujibu , sio tu mbele ya bunge bali pia kwa raia wa Afrika Kusini, wakosoaji wake wanasema

Kwa kuzingatia misimamo mikali ya vyama vya upinzani ambavyo baadhi yao vinamtaka aachie ngazi mara moja, kashfa hii ina uwezo wa kumgharimu kazi yake.

Katika wasilisho la kurasa 138 lililowasilishwa kwa jopo hilo, Rais Ramaphosa alikanusha kuwa kulikuwa na kitu kibaya kuhusu pesa zilizofichwa kwenye shamba lake la kibinafsi, akisema zilitokana na mapato ya nyati waliouzwa kwa dola 580,000 taslimu kwa raia wa Sudan, Mustafa Mohamed Ibrahim Hazim, mwishoni mwa 2019.

Hata hivyo, Bw Hazim hajajitokeza hadharani na ni machache yanayojulikana kumuhusu.

Jopo hilo lilihoji kwa nini stakhabadhi iliyowasilishwa kwao haikuwa na maelezo yoyote ambayo yangemfanya atambulike. Kulikuwa na jina lake tu, hakuna anwani ya biashara wala nambari ya kitambulisho.

Kwa heshima nasema mashtaka yote nilioitwa kuyajibu hayana msingi wowote , bwana Ramaphosa aliandika, akiongezea kwamba madai mengi yalikuwa uvumi . Aliomba kwamba suala hilo lisiendelezwe.

Lakini halijamuondokea na kuna shinikizo kwa rais kujiuzulu au ashtakiwe bungeni.

Ni vigumu kukosa kejeli ya madai na hali ambayo Rais huyo anijikuta.

Hii ni baada ya kiongozi huyo ambaye taswira yake ya kisiasa na kupanda madarakani hadi kuwa rais kulijengwa kutokana na vita vyake dhidi ya ufisadi, ambao ulitawala chama tawala cha African National Congress (ANC) na nchi nzima kwa ujumla chini ya mtangulizi wake Rais Jacob Zuma. Wito wa Uchaguzi wa mapema

Je, ni nini basi kifanyike kwa jinsi Bw Ramphosa alivyoshughulikia sakata ya "Farmgate"?

Chama chake kinajadili kwa ukali jinsi rais anapaswa kushughulikia ripoti hiyo, vyanzo vya chama vimeiambia BBC.

Wakati wengine wanamtaka achukue mbinu ya kusubiri na kuona, wengine, kutoka kwa kundi pinzani la ANC, wanamtaka aondoke ili kuzuia uharibifu zaidi kwa chama, wanasema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live