Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kansiime ajifungua mtoto wa kiume

Screenshot 2021 04 25 At 10.30.13 660x400.png Kansiime ajifungua mtoto wa kiume

Sun, 25 Apr 2021 Chanzo: millardayo.com

Mchekeshaji maarufu toka nchini Uganda, Anne Kansiime amejifungua mtoto wa kiume jana Jumamosi Aprili 24, 2021 na kumpa jina la Selassie.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Anne (34) alithibitisha kujifungua kwa ku-share picha inayomuonyesha akiwa kitandani ndani ya hospitali aliyojifungulia mwanae huyo, akionekana kumbembeleza na kusema kuwa anaitwa “Selassie Ataho”.

Pia aliongeza maneno yanayosomeka, “dhambi zake zimesamehewa” Hii ni kama amewakata ngebe mahasimu wake, baada ya kuandamwa kwa muda mrefu na maneno ya kuwa hawezi kushika ujauzito.

Selassie anakuwa mtoto wa kwanza kwa Kansiime na mpenzi wake Abraham Tukahiirwa.

AWILO LONGOMBA USO KWA USO NA JOSEPH KUSAGA, AZUNGUMZA HAYA

Chanzo: millardayo.com