Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kanisa laongoza maandamano dhidi ya waasi wa M23 DRC

Kanisa Laongoza Maandamano Dhidi Ya Waasi Wa M23 DRC Kanisa laongoza maandamano dhidi ya waasi wa M23 DRC

Mon, 5 Dec 2022 Chanzo: Bbc

Maelfu ya watu kote katika jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo wameshiriki katika maandamano ya kupinga kundi la waasi wa M23 – mojawapo ya makumi kadhaa ya wasi wanaoigania mashariki mwa nchi hiyo.

Kanisa katoliki limewaita watu kushiriki kufanya maandamano kwenye mitaa na hasira zaidi ilielekezwa kwa Rwanda ambayo Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo inaishutumu kwa kuwaunga mkono wasi wa M23 - kitu ambacho Rwanda inakikanusha.

Baada ya kumaliza ibada ya Jumapili kote nchini , walifanya maandamano ya amani.

Kanisa Katoliki lina ushawishi mkubwa nchini humo. Baadhi ya viongozi wa kanisa hilo wanatoa wio kwa nchi za Magharibi kuchukua msimamo mkali dhidi ya serikali ya Rwanda kwa kuwaunga mkono wasi wa M23.

Mabango katika maandamano mjini Kinshasa yalionyesha kupinga kile kinachodaiwa kuwa ni kugawanywa kwa DRC kulingana na makabila kuna tekelezwa na mataifa mengi na pia yalielezea kuhusu unafiki wa jamii ya kimataifa.

Mazungumzo ya kikanda yamekuwa yakifanyaika kujaribu kuzuia vurugu.

Nchi kadhaa za Afrika Mashariki zinawatuma wanajeshi wake lakini katika miaka iliyopita kuhusika kwa majeshi ya mataifa mengi kuliufanya mzozo kuwa mgumu zaidi katika eneo hilo la mashariki mwa DRC lenye utajiri wa madini.

Chanzo: Bbc