Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kanisa lamtoza faini aliekutwa akifanya mapenzi kanisani, jamaa atoweka

Kanisa Kanisa Kanisa lamtoza faini aliekutwa akifanya mapenzi kanisani

Thu, 13 Jul 2023 Chanzo: Mwananchi

Mwanaume Wilaya ya Kayunga nchini Uganda (jina linahifadhiwa), ametozwa faini ya Sh600, 000 kwa madai ya kufanya mapenzi na mpenzi wake kwenye mimbari ya kanisa.

Wakazi wa mji huo wameuambia mtandao wa Monitor kuwa wiki iliyopita, waliwapata wawili hao wakifanya kitendo hicho ndani ya jengo jipya la kanisa la Bugonya katika Kaunti Ndogo ya Kayonza nchini humo.

Tukio hilo lilitengeneza vichwa vya habari kwa ‘utatu’ wake usio wa kawaida kwani mwanamume Mkatoliki alikutwa akifanya mapenzi na mwanamke Mwislamu kwenye madhabahu ya Kanisa la Anglikana.

Wawili hao walipelekwa hadi kwa Afisa namba moja moja wa eneo hilo (LC1), ambapo waliachiliwa wakisubiri kusikilizwa kwa kesi yao, hata hivyo, mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 23 ametoweka.

Inasemekana mwanaume huyo anajificha kwa rafiki yake katika kijiji hicho, huku mwanamke ambaye ni ametalakiwa, akiwa amechukuliwa na mama yake.

Aidha, kutokana na shikizo kutoka kwenye jamii ya maeneo hayo, lakini pia kwa kutoka kwa Polisi na familia yake, baba wa mwanaume huyo amejitokeza na kuwasihi viongozi wa eneo hilo kwamba adhabu ya Sh600,000 ilikuwa nje ya uwezo wao.

Taarifa za awali zinaonyesha kuwa wapenzi hao waliruka ukuta na na kuingia ndani ya kanisa hilo jioni ya siku ya tukio wakipitia dirisha ambalo ujenzi wake ulikuwa bado haujakamilika.

Uongozi wa kanisa na kijiji uliamua kwamba kama adhabu, basi washukiwa hao walitakiwa kuweka ‘shutters’ kwenye madirisha yote ya jengo hilo la kuabuadia, ambayo bado hayajakamilika.

Chanzo: Mwananchi