Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kanisa la Orthodox lamkosoa waziri mkuu Ethiopia

Fn8skn1XwAAxO7O.jpeg Kanisa la Orthodox lamkosoa waziri mkuu Ethiopia

Thu, 2 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uongozi mkuu wa Kanisa la Kiorthodox nchini Ethiopia (Synodi), ambalo ni Kanisa kubwa zaidi la Ethiopia, umetishia kuitisha mikutano ya kitaifa itakayoongozwa na mkuu wa Kanisa Hilo, Abuna Mathias.

Kanisa hilo limekosoa kauli za hivi karibuni za waziri mkuu kuhusu makasisi wakorofi waliohusika katika uteuzi wa maaskofu bila uelewa.

Hotuba ndefu ya Bw Abiy, iliyotangazwa kwenye televisheni ya taifa, ilitolewa baada ya sinodi ya kanisa hilo kuwatenga makasisi, ambao wanatoka katika jimbo la Oromia nchini humo.

Aliwaonya mawaziri wake dhidi ya kujihusisha na masuala ya kanisa. Hatahivyo, alisema kila upande ‘’una ukweli.”

Sinaodi ilisema kuwa kauli za Waziri mkuu zilipuuza maamuzi yake na kukosoa mamlaka yake na kulitambuakundi “lisilo halali lenye njaa ya madaraka.

Baadhi ya kauli za Bw Abiy zilikuwa "zinapotisha", iliongeza.

Kundi la maaskofu waliojitenga linalishutumu kanisa kwa kushikilia mfumo wa lugha na utamadunina mamlaka ambapo kanisa la Oromia waumini hawafundishi kwa lugha zao zaq asili. Kanisa limekanusha shutuma hizo.

Makasisi waliojitenga walisema “walizidiwa ” na uungaji mkono wa umma baada ya kutembelea baadhi ya maeneo katika jimbo llililokumbwa na mzozo la magharibi mwa Oromia.

Taarifa ya sinodi inakuja huku kukiwa na shutuma miongoni mwa waumini kwamba mamlaka zinawaunga mkono makasisi waliojitenga.

Uhisano baina ya utawala wa Bw Abiy na kanisa – lenye waumini karibu nusu ya milioni 110 ya raia wa Ethiopia umekuwa ukizorota licha ya kwamba ulikuwa mzuri katika siku za mwanzo za uongozi wake.

Katika miaka ya hivi karibuni waumini wake wamekuwa wakiripotiwa kulengwa.

Uhusiano wa pande mbili ulizorota zaidi wakati wa vita vya Tigray baada ya Askofu Abuna Mathias kuzungumza dhidi ya kile alichokiita mauaji ya kimbari (genocide) katika jimbo hilo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live