Seneta Kang'ata alisema alimuonya Rais Uhuru kupitia barua yake tata kuhusu BBI kuwa baadhi ya viongozi wa Jubilee watagura chama hicho kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2022 Mbunge huyo alisema baadhi ya viongozi kutoka ngome ya Uhuru, Mlima Kenya wanachukuwa muda wao kabla ya kuhamaMbunge wa Nyeri Town Ngunjiri Wambugu ametabiri kuwa chama cha Jubilee kitawapoteza wanachama wengi iwapo hakita kaza kamba
Seneta wa Murang'a, Irungu Kang'ata amesherehekea baada ya baadhi ya wanachama wa Kieleweke kuhamia katika kambi ya Naibu Rais William Ruto.
Katika taarifa kwenye ukurasa wake wa Twitter, Jumatano, Juni 23, Kang'ata alisema alimuonya Rais Uhuru kupitia barua yake tata kuhusu BBI kuwa baadhi ya viongozi wa Jubilee watagura chama hicho kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2022.
Katika barua hiyo, Mbunge huyo alisema baadhi ya viongozi kutoka ngome ya Uhuru, Mlima Kenya wanachukuwa muda wao kabla ya kuhama.
"Muheshimiwa, katika barua yangu ya Januari 2021, nilikuonya mambo mengi. Mwanzo, BBI ni shida ilitimia kupitia uamuzi wa korti. Pili kuna Komorera (wanasiasia wasiokuwa na msimamo) wanaokuzingira na sasa inatimia," Kang'ata aliandika.
Wa Muchomba ambaye alikuwa katika mrengo wa Rais Uhuru Kenyatta wa Kieleweke katika chama cha Jubilee amehiadi kuabiri wilbaro na tayari amekutana na Naibu Rais nyumbani kwake mtaani Karen.
Kando na Wa Muchomba, wabunge wengine waliohama ni David Gikaria (Nakuru Town East) na Samwel Gachobe (Subukia).
Mbunge wa Nyeri Town Ngunjiri Wambugu ametabiri kuwa chama cha Jubilee kitawapoteza wanachama wengi iwapo hakita kaza kamba.
"Vile mambo yako kwa sasa sitashangaa hata tukiwapoteza wachezaji zaidi. Tuko na kazi ngumu mbele yetu ya kusuluhisha mambo ndani ya chama na ninajua si kila mtu yuko tayari kufanya hilo," alisema Wambugu.
READ ENGLISH VERSION
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 073248269.
Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke