Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kanali wa DR Congo ahukumiwa kifo

Kanali Wa DR Congo Ahukumiwa Kifo Kanali wa DR Congo ahukumiwa kifo

Tue, 3 Oct 2023 Chanzo: Bbc

Kanali wa jeshi amehukumiwa kifo katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa kuhusika katika mauaji ya zaidi ya waandamanaji 50 mwezi Agosti.

Wanajeshi wanaohudumu chini ya Mike Mikombe walifyatua risasi katika mji wa mashariki wa Goma dhidi ya wafuasi wa madhehebu ya kidini walioshiriki katika maandamano yaliyopigwa marufuku wakipinga kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa.

Alishtakiwa kwa uhalifu dhidi ya binadamu.

Maafisa wenzao watatu pia wamefikishwa katika mahakama ya kijeshi na kuhukumiwa kifungo cha miaka 10 jela.

Mawakili wa Kanali Mikombe wamesema watakata rufaa.

Hukumu ya kifo hutolewa nchini DR Congo lakini imepita zaidi ya miaka 20 tangu mtu anyongwe.

Chanzo: Bbc