Wed, 30 Aug 2023
Chanzo: Bbc
Kampuni ya Ufaransa ya uchimbaji madini Eramet imeripotiwa "kusimamisha" shughuli zakei nchini Gabon kufuatia mapinduzi ya kijeshi.
Kampuni hiyo ilisema kuwa imesitisha kazi "kwa kuzingatia usalama wa wafanyikazi na usalama wa operesheni", shirika la habari la AFP linaripoti.
Kampuni hiyo inaajiri takriban watu 8,000 katika nchi hiyo yenye utajiri wa madini, koloni la zamani la Ufaransa.
Kampuni yake tanzu huchimba madini ya manganese kutoka migodi ya Moanda, migodi mikubwa zaidi ya manganese duniani. Madini hutumiwa katika utengenezaji wa chuma na betri.
Chanzo: Bbc