Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kampuni ya Kenya Power kuanza kutoa umeme kwa mgao

Kampuni Ya Kenya Power Kuanza Kutoa Umeme Kwa Mgao Kampuni ya Kenya Power kuanza kutoa umeme kwa mgao

Thu, 14 Dec 2023 Chanzo: Bbc

Kampuni ya Kenya Power itaanza kutoa umeme kwa mgao, ikilenga eneo maeneo tofauti nchini ili kupunguza shinikizo dhidi ya miundombinu ya umeme iliyozeeka ambayo inatatizika kukidhi ongezeko la ghafla la mahitaji.

Katika taarifa,kampuni hiyo imesema kuwa mpango wa kutoa umeme kwa mgao utaathiri kaunti za Kiambu, Machakos, Kajiado, Embu, Nyeri, Uasin Gishu, Nandi, Kisii, Migori na Kilifi. Maeneo hayo yatakuwa bila umeme kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa moja usiku.

Haya yanajiri baada ya Wizara ya Kawi kutangaza msururu wa hatua zinazokusudiwa kupunguza matatizo ya mara kwa mara ya umeme nchini, kisa cha hivi punde zaidi kikiwa Jumapili usiku.

Mapema wiki hii, Waziri wa Kawi Davis Chirchir alisema usambazaji wa kawaida wa umeme ulisababishwa na mahitaji makubwa ya umeme, ambayo yalisababisha njia ya ugavi wa umeme katika eneo la magharibi mwa kenya kukatika.

Waziri Chirchir alihusisha changamoto hiyo na ukosefu wa uwekezaji katika uzalishaji wa umeme na usambazaji wake.

Chanzo: Bbc