Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kampuni ya Bahrain kuuza mafuta Uganda

UNOC UGANDA (600 X 343) Kampuni ya Bahrain kuuza mafuta Uganda

Fri, 3 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kampuni ya Bahrain, Vital Energy itaanza kuingiza mafuta ya petroli nchini Uganda ikiwa ni hatua mpya ya taifa hilo la Afrika Mashariki kuondoa utegemezi wake wa mahitaji ya mafuta kutoka kwa taifa jirani la Kenya.

Waziri wa Nishati wa Uganda aliwasilisha mswada mbele ya bunge kutaka kutoa haki za kipekee kwa kampuni ya Bahrain Vitol kuwa mwingizaji pekee wa bidhaa za petroli nchini humo.

Baraza la mawaziri la Uganda tayari limeidhinisha mabadiliko ya sheria ya mafuta ya petroli.

Mkataba kati ya Kampuni ya Kitaifa ya Mafuta ya Uganda (UNOC) inayomilikiwa na serikali na Vitol Energy tayari upo.

Chini yake, Vitol itasambaza bidhaa za mafuta kwa Kampuni ya Kitaifa ya Mafuta ya Uganda ambayo nayo itauza bidhaa hizo kwa waendeshaji wa vituo vya mafuta. Usafirishaji wa kwanza kutoka Vitol unatarajiwa kuwasili Januari, 2024.

Vitol na UNOC zitaanzisha "hifadhi za akiba" nchini Uganda na Tanzania ili kuhakikisha usalama wa usambazaji wa mafuta nchini Uganda.

Kulingana na msemaji wa Wizara ya Nishati, Vitol na UNOC walikuwa tayari wametia saini makubaliano hayo.

Baadhi ya makampuni ya uuzaji wa mafuta yamekosoa mpango huo, na kuishutumu serikali ya Uganda kwa kutaka kuunda ukiritimba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live