Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kampuni tatu zaondolewa

6f07baf8c7fdff509e5873a7f850f510 Kampuni tatu zaondolewa

Tue, 13 Oct 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

KAMPALA

KAMPUNI tatu za biashara ya mchele zimeondolewa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), ili kuingiza bidhaa hiyo kwa wingi nchini kukabiliana na upungufu wa mchele uliosababishwa na mlipuko wa ugonjwa wa covid-19.

Kampuni zilizoondolewa kodi hiyo ni Gotovate Uganda Limited, Williex Commodities Limited na Akhcom Limited na tayari zimepewa kibali na Wizara ya Fedha na ya Biashara kuingiza mchele nchini.

Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wa Mchele, Isaac Kashaija, mwishoni mwa wiki alisema kwa sasa mahitaji ya mchele nchini ni takribani tani 380,000 kwa mwezi, wakati uzalishaji wa ndani ukiwa ni tani 180,000 kwa msimu, hivyo kuwa na upungufu wa tani 200,000 kwa mwezi.

Kiwango kikubwa cha mchele huingizwa nchini kutoka Tanzania na Pakistan kutokana na mpunga unaozalishwa nchini Uganda kuwa na ubora wa chini.

“Kama tunahitaji mchele wa kutosha inatakiwa kusaidia wakulima kupanda mpunga mwingi au kuongeza ubora na wingi wa uzalishaji mpunga kulingana na mahitaji, lakini kabla ya kufanya hivyo ni lazima kuruhusu kuingiza mchele nchini kutoka nje,” alisema.

Kashaija alisema kutokana na upungufu huo, kampuni ya Gotovate Uganda Limited imeruhusiwa kuingiza tani 50,000 za mchele kutoka Tanzania bila kulipa VAT na msamaha huo ni kwa kipindi cha Agosti mpaka Desemba, mwaka huu.

Hatua ya kuondolewa kodi hiyo kwa kampuni ya Gotovate imepokewa kwa mawazo tofauti na wadau, baadhi wakidai itaathiri soko la ndani la mchele, lakini Kashaija alitetea kuwa itasaidia kukabiliana na upungufu wa bidhaa hiyo nchini.

Alisema mwaka 2014 serikali ilisamehe kodi kwa kampuni 14 za mpunga baada ya kulalamikiwa na Bunge kuhusu msamaha wa kodi katika kuingiza mchele kutoka Tanzania na nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na kufaikiwa kuingiza bidhaa hiyo kutoka nje kwa miaka sita iliyopita kwa msamaha wa kodi ya Sh trilioni moja.

Chanzo: habarileo.co.tz